Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa leo tumeambiwa tarehe ya utekelezaji wa mradi huo na kwa kuwa kabla ya hapo tuliahidiwa kwamba mwezi wa Tatu mradi huu ungekuwa tayari.

Je, wananchi wa Vijiji hivyo kwenye Wilaya ya Rungwe wategemee kauli gani ya Serikali ya kuhakikisha hili jambo linakamilika kwa uweli baada ya miezi mitatu?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili; Kijiji cha Ikombe Wilayani Kyela kilishafanyiwa uhakiki na kuwekea peg lakini mpaka sasa hivi hakuna dalili zozote za kupelekewa umeme wa REA: Je, ni lini Serikali itapeleka umeme huko?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na Mheshimiwa Ally Jumbe kwa niaba ya Mheshimiwa Mwantona, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza ni kweli kwamba tulitarajia kumaliza mradi huu mapema lakini kama mnavyofahamu kulitokea ongezeko na mabadiliko makubwa sana ya bei na hivyo hata baada ya ukamilishaji wa kuangalia upungufu uliokuwa umejitokeza, tumeingia katika negotiation ya kuhakikisha kwamba tunapata fedha halisi ya kuweza kuongeza ili tumalize mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawaahidi wananchi wa maeneo hayo kwamba baada ya kukamilisha mchakato wa kukubaliana bei halisi ya ongezeko la vifaa, sasa tupo tayari kwenda kupeleka umeme katika maeneo hayo kwa kurekebisha yale maeneo ambayo yalikuwa yamebakia.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali la pili. Katika kijiji hicho ambacho kimesemwa na vijiji vingine vyote ambavyo vipo Tanzania bara kama tulivyosema, vitapelekewa umeme kufikia Desemba mwaka huu kama ahadi ya Mheshimiwa Rais kwenye Ilani ilivyotolewa.

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kutokana na matatizo mbalimbali wanayopata wananchi wanaotumia umeme nje ya Gridi ya Taifa, mwezi wa Pili mwaka huu Wizara iliunda timu ya wataalam ikiongozwa na Mheshimiwa Naibu Waziri kuzungukia maeneo haya kusikiliza wananchi na baadaye kutoa uelekeo nini utatuzi wa changamoto zile, lakini tokea wakati huo mpaka sasa Wizara imekuwa kimya. Wananchi, wakiwemo wananchi wa Jimbo la Ukerewe Visiwa vya Gana na Ukara wanataka kusikia nini maelekezo na uelekeo wa Serikali juu ya changamoto hizi? Nashukuru.

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mimi mwenyewe nilifika Nansio, Ukerewe; nilifika Ukara, Gana, Kamasi, Irugwa katika visiwa vyote vya Ukerewe ili kuangalia changamoto ambayo wananchi wanaipata. Maeneo haya yapo mengi zaidi. Yalikuwepo mengine katika Mkoa wa Kagera na mengine katika maeneo ya Buchosa. Zoezi lile linaendelea na tunatarajia litakamilika mwishoni mwa mwezi huu. Litakapokuwa limekamilika, taarifa ya Serikali na maelekezo ya Serikali yatatolewa kwa maeneo yote ambayo yalikuwa na changamoto ya bei ya umeme na wananchi wataendelea kupata umeme kwa gharama ambazo ni nafuu ili Serikali iweze kuwahudumia vizuri.

Name

Edwin Enosy Swalle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 3

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi. Jimbo la Lupembe katika Vijiji vya Lyalalo, Mfiriga, Itambo, Madeke na Kanikelele wamepata umeme wa REA, lakini tangu mwaka 2021 zimewekwa nguzo na hakuna ambacho kinaendelea. Wananchi hawa wangependa kujua nini mpango wa Serikali kufunga umeme hayo maeneo ambayo wananchi wangu wana nguzo? Ahsante. (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Swalle, Mbunge wa Lupembe kama ufuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyosema hapo awali, kulitokea mabadiliko makubwa sana ya vifaa vya dukani hasa vinavyotengenezwa kwa kutumia chuma, alminium na Copper. Tumemaliza mazungumzo sasa ya kuona gharama ambazo zimeongezeka na Serikali inayo fedha ya kuongeza katika utekelezaji wa mradi huu, kutoka ile Shilingi trilioni 1,250.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika muda mfupi ujao wakandarasi watarudi site wakiwa sasa wamepata fedha ya nyongeza ya kununua vile vifaa ambavyo gharama zake zilikuwa zimepanda na mradi utaendelea kama uvyoanza na plan ilivyo.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 4

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa kwenye mradi wa scope hii ya mwisho ya round III ya REA tuliongeza proposal ya kuongeza vijiji, hamlets na institutions, tukaipeleka REA na TANESCO kwa ajili ya utekelezaji, lakini tuliruka chanzo cha maji cha Kijiji cha Njomlole:-

Je,Serikali inaweza ikatuorodheshea Kijiji hicho pia ambacho kilirukwa kwa bajati mbaya ili kiingie katika mradi utakaokuja kwa vijiji tulivyoomba viongezwe na miradi?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ni eneo la kijiji, vijiji vyote vimechukuliwa na vipo kwenye mpango wetu wa REA III round II na umeme utafika katika eneo hilo. Ila nimesikia kwamba ni kwenye chanzo cha maji; upo mradi mahususi wa kupeleka umeme kwenye vyanzo vya maji, kwenye migodi na kwenye vituo vya afya. Tunazo site zaidi ya 560 ambazo zimechukuliwa katika bajeti inayokuja, tutaiweka eneo hilo kuwa mojawapo la kupelekewa umeme ili wananchi waweze kuendelea kupata huduma. (Makofi)

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 5

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ina changamoto kubwa sana ya kukamilika kwa miradi ya REA hususan kwenye Kata za Bangata, Oltroto na Lengijave; na hii imetokana na kubadilishwa kwa wakandarasi: -

Je, Serikali itatatua vipi changamoto hii?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, huko nyuma tulikuwa tuna utaratibu wa kutekeleza mradi uliokuwa unaitwa GOODS. Tunampa makandarasi fedha, anakwenda ananunua vifaa; kwenye mkataba unakuta asilimia 80 ni vifaa, asilimia 20 ndiyo labour. Akishanunua vifaa akapata faida yake, anaondoka, anatelekeza mradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mradi huu tunaoutekeleza sasa, tumebadilisha utaratibu. Tunafanya kwa utaratibu unaoitwa WORKS. Tunamlipa mkandarasi kulingana na kazi aliyoifanya. Hatutarajii kuwepo na utelekezaji wa miradi wala kushindwa kukamilika kwa miradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile hiyo ya nyuma, tumeongeza usimamizi. Kama mnavyofahamu, wasimamizi tangu ngazi ya Jimbo kuja kwenye Mikoa tunahakikisha kwamba miradi yote inakamilika kwa kadri tulivyojipangia.

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 6

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa Mkoa wa Kigoma tulichelewa kupata umeme wa awamu ya kwanza na ya pili: Je, katika awamu wa tatu mzunguko wa pili, Serikali ipo tayari kumsimamia mkandarasi ili umeme uweze kufika vijijini na katika vitongoji vyote? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Josephine Genzabuke, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kauli ya Serikali na ahadi ya Serikali ni kusimamia wakandarasi bega kwa bega kuhakikisha kwamba miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa kadri tulivyojipangia. Usimamizi huu ni wa vitendo; wapo wasimamizi kwenye ngazi za Jimbo wanakuja, wapo wasimamizi kwenye Kanda, wapo wasimamizi ngazi ya Taifa, na watu wote wamewezeshwa kuhakikisha kwamba kazi hizi zinafanyika na kukamilika kwa wakati.

Name

Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 7

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nataka kujua tu kujua kuhusiana na suala la REA Awamu ya III ujazilizi. Kwenye Jimbo langu la Mchinga, nilibakiza vijiji 12. Naipongeza Serikali wamenipatia, lakini sambamba na hilo, kuna nguzo zimewekwa, sasa ni zaidi ya miezi sita hakuna kinachoendelea. Nini kauli ya Serikali? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Salma Kikwete, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakiri kwamba tulipata changamoto kidogo ya miradi kutoendelea kwa kasi na speed tuliyoitarajia kwa sababu ya mabadiliko ya bidhaa za viwandani. Tunasema kwamba nguzo zilipatikana kirahisi, ni kwa sababu tulipolipa ile advace payment asilimia 20, Wakandarasi walitumia asilimia 15 kwenda kununua vifaa ambavyo vinapatikana hapa hapa nyumbani zikiwemo na nguzo. Kuja kuingia kwenye awamu ya pili ya kununua vifaa ambavyo vinatoka madukani, ndiyo sasa bei zimepanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, baada ya mazungumzo na committment ya Serikali ya kuongeza fedha, matatizo yote haya ya nguzo zilizosimama bila kuwekewa nyaya na transforma, zinaenda kwisha na kazi itaendelea kwa kasi kubwa zaidi. (Makofi)

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 8

MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa mpango wa REA kwa Mkoa wa Singida mpaka mwezi wa Saba wanatakiwa wawe wameunganisha vijiji 10 na umeme, lakini katika Wilaya ya Ikungi Majimbo ya Singida Magharibi na Mashariki vijiji saba vyote ni vya Jimbo la Singida Mashariki: -

Je, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaongeza idadi ya vijiji katika Jimbo la Singida Magharibi kutoka vitatu na kuendelea ili wananchi wapate huduma ya umeme? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi hii tunayoitekeleza inalenga kupeleka huduma kwa wananchi. Kwa hiyo, kama kijiji kimepata umeme kwenye mradi mmoja, kwa mfano vijiji alivyovisema saba vimepata umeme kutoka kwenye mradi wa backborn wa Mradi wa msongo wa kilovolt 400 kwenda Namanga, then vimeshapata umeme. Vile vijiji vingine vyote vilivyobaki ndiyo vinaingizwa kwenye REA III round II. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hakuna kijiji hata kimoja kitakachobaki bila kupata umeme; kama hakipo kwenye REA III basi kitakuwa kipo kwenye mradi mwingine kwa ajili ya kpatiwa umeme. (Makofi)

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 9

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mbulu Vijijini kuna kata tatu ambazo hazina umeme na vijiji 15. Nakubali majibu ya Mheshimiwa Waziri kwamba REA wameondoka site kutokana kupanda umeme na kupanda gharama za umeme: -

Je, ni lini mnamaliza huo utaratibu wa kukubaliana na hao wakandarasi ili warudi site wakakamilishe mradi huu wa REA?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Flatei, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi mwenyewe nilienda katika Jimbo lake kuzindua umeme katika REA III round II na kazi ilikuwa inaendelea. Kama alivyosema, ni kweli tulikuwa na changamoto hiyo, lakini tayari tumeshakamilisha taratibu za mazungumzo, na wakati wa maonesho hapa Mheshimiwa Waziri aliwaambia wakandarasi wote Serikali tayari imeshatoa fedha kwa ajili ya kuongeza ile nakisi iliyokuwepo. Kwa hiyo, wakandarasi wanarudi site kwa ajili ya kuendelea kufanya kazi wakiwa na uhakika kwamba Serikali ya Awamu ya Sita itatoa fedha ili kazi iweze kukamilika.

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: - Je, ni lini Mradi wa REA II wenye vijiji 25 na REA III wenye vijiji 33 utakamilika katika Jimbo la Rungwe?

Supplementary Question 10

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wilaya ya Kyerwa ina vijiji 29 ambavyo bado havijapatiwa umeme ikiwemo Kata ya Nkwenda Kijiji cha Kakerere, Kata ya Kakanja Kijiji cha Keshanda na Kata ya Lukolaijo Kijiji cha Mgorogoro. Navitaja hivi kwa sababu vipo mjini. Ni lini hivyo vijiji vitapatiwa umeme? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anatropia, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni committment na Serikali kwamba itakapofika Desemba mwaka huu vijiji vyote viwe vimepelekewa umeme mabadiliko na nyongeza kidogo itatokana na changamoto ambazo wakati tunawasilisha bajeti tulizisema. Ila Kyerwa ni eneo mojawapo ambalo mkandarasi yupo site na kazi zinaendelea na tunaamini kwamba kazi itakamilika kwa jinsi tulivyojipangia. (Makofi)