Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Old Shinyanga kupitia Iselamagazi, Solwa hadi Salawe kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imeshakamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kipande cha kutoka Solwa kwenda Salawe kilomita 15, je, ni lini ujenzi utaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa sehemu ya Solwa – Iselamagazi yenye kilomita 64.66, upembuzi unaendelea. Je, ni lini huo upembuzi utakamilika ili ujenzi uanze? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Christina Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa utaratibu uliopo ni kwamba, kwa kuwa barabara hii ni moja itakuwa na lot moja kwa hiyo tunataka tupate tathmini ya gharama ya barabara nzima ili tuweze kupata gharama ya barabara nzima na kuianza kuijenga kwa kiwango cha lami kwa jinsi itakavyokwenda. Kwa barabara hii ambayo imebaki kilomita 64.66 kama tulivyosema, usanifu na upembuzi yakinifu unaendelea, tunategemea utakwenda kadri ya mkataba ulivyopanga na tunaamini kwamba kabla ya mwisho wa mwaka huu 2022, usanifu utakuwa umekamilika. Ahsante.