Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza:- Je, kwa nini Serikali imewaacha wananchi wengi wenye sifa na vigezo vya kunufaika na TASAF katika Jimbo la Mwibara?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa vile mfumo wa TASAF katika Jimbo la Mwibara umekufa, matatizo ni mengi, malalamiko ni mengi; je, ni lini Serikali itafanya upya zoezi la kuwatambua wanufaika?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kumjulisha Mbunge na pia kulijulisha Bunge lako kwamba mfumo wa TASAF haujafa. Tunazo changamoto katika maeneo mbalimbali ambayo kweli yako matatizo hasa katika eneo la utambuzi na uandikishaji wa wanufaika hao.
Mheshimiwa Spika, nataka nirudie tena kuendelea kuwasisitiza Waheshimiwa Wabunge na Bunge lako kwamba kama liko tatizo lolote, ofisi zetu zipo kwa ajili ya kusikiliza na kama taratibu zetu zinavyoeleza, kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri yeyote, basi rufaa zitapelekwa hapo na taratibu kwa ajili ya kutatua matatizo au changamoto zinazotokea yatafanyika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved