Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya mapitio ya viwango vya malipo ya ujira kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii Mlima Kilimanjaro?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, naomba niulize swali moja la nyongeza, ila niruhusu nijieleze kidogo.

Mheshimiwa Spika, wakati kunatokea moto kwenye mlima watu wanaokimbizana kuuzima ni wale wanaoishi kandokando ya ule mlima; pale Marangu wanabebwa, wanasombwa, wanalazimishwa kwenda kuzima moto. Sasa tulikuwa tunaomba Serikali itoe kauli kuhusiana na uwezekano wa kutoa mwongozo ili wale tour operators wawe na uwiano fulani tuseme asilimia 70 ya wahudumu wanaopandisha watalii wawe wanatoka kwenye eneo lile la pale Marangu. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na tunaenda kuufanyia kazi tuone ushauri wa kitaalam utatuelekeza vipi. (Makofi)