Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Primary Question

MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kununua pamba toka kwa wakulima pindi bei ya pamba inapoporomoka katika soko la dunia?

Supplementary Question 1

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza ninakubaliana na majibu ya Serikali, wamefanya analysis vizuri lakini jinsi bei inavyopanda katika soko la dunia kama Serikali ilivyoeleza, hata gharama za ulimaji au za kilimo zinapanda vile vile.

Je, kwa nini basi Serikali isiangalie namna ya ku-subsidize hili zao la pamba kwamba mkulima anapolima ukatengeneza bei fulani ambayo kama itashuka katika bei ya dunia basi mkulima huyo aweze kuuza kwa bei ambayo imepangwa hata kabla hajaenda kwenye kilimo, kwa sababu analima kwa gharama kubwa wakati wa kuvuna bei inakuwa imeshuka na inawaumiza sana wakulima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mmesema wenyewe mtakuja na kitu kinaitwa price stabilization fund, mtatunga sheria mtaileta Bungeni.

Je, ni lini sheria hiyo itatungwa ili sisi wadau wa pamba tuweze kuchangia katika sheria hiyo na tuje na sheria ambayo ni nzuri kwa mkulima wa pamba nchini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, cha kwanza nikubaliane vile vile na maoni ya Mheshimiwa Mbunge ya kuhakikisha tuna-subsidize katika zao la pamba katika kuhakikisha tunamsaidia mkulima. Sisi kama Serikali jambo hili tumelipokea. Tunachofanya ni tathmini, tutatafuta fedha ili kuhakikisha jambo hili linafanikiwa na kuwa lenye mantiki kwa faida ya wakulima wote wa pamba nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lini sheria hiyo tutaleta, nafikiri kwa sababu tupo katika mchakato wa kuanzisha huu mfuko wa kinga ya bei. Tutakapomaliza huu mchakato ninaamini kabisa kwamba kabla hatujafika mwaka 2025 jambo hili litakuwa limekamilika na limeanza kufanyiwa kazi.

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kununua pamba toka kwa wakulima pindi bei ya pamba inapoporomoka katika soko la dunia?

Supplementary Question 2

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi, Mbunge wa Lupembe, Mheshimiwa Swalle amekuwa akihangaika sana na wananchi wake juu ya chai. Sasa, tangu juzi viwanda vya chai kule Lupembe vimesimama, wakulima hawana mahala pa kwenda kuuza chai kule Lupembe.

Je, ni lini Serikali itatupa jibu la viwanda vile viweze kufanya kazi wakulima waweze kuuza chai yao?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jambo hili sisi kama Wizara tunalifahamu na Waziri wa Kilimo tayari ameshatuma timu ya wataalamu kwenda kushughulikia changamoto hiyo. Kwa hiyo, mara baada ya kurudi kwa tume hiyo tutakuwa katika nafasi ya kujibu na kuwasaidia wakulima wa Lupembe hususani wa zao la chai. Kwa hiyo jambo hili tunalifahamu na tunalifanyia kazi; na Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan haitaacha jambo hili liende ili kuwaumiza wakulima wa chai nchini.

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Primary Question

MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kununua pamba toka kwa wakulima pindi bei ya pamba inapoporomoka katika soko la dunia?

Supplementary Question 3

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa sababu kubwa ya kushuka kwa bei ya pamba ni makato makubwa yanafanywa na Bodi ya Pamba, ambapo mwaka 2021 kwa kilo moja walikata shilingi 400; mwaka 2022 walikata shilingi 300 kwa kilo moja; na mwaka huu 2024 napo watakata.

Je, ni nani anayeruhusu viwango hivi kukatwa na kusababisha wananchi kupata bei ndogo ya pamba?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninafahamu Mheshimiwa Mpina anatambua kwamba kuna makato ambayo yapo katika kanuni, kuna makato ambayo wakulima wanakubaliana wao wenyewe na kuna makato ambayo yapo kisheria. Kwa hiyo sisi ambacho tunakipokea ni kwamba, panapotokea malalamiko kila baada ya msimu wa zao ambalo linakuwa limelimwa ama limefanyiwa biashara, Wizara tunakuwa tunapitia na kuangalia yale makato. Yale ambayo tunaona yanamuumiza mkulima tunashauri Bunge lako Tukufu tunayaondoa. Kwa hiyo sisi jambo hili tuseme tumelipokea na baada ya huu msimu utapokwisha basi tutapitia yale makato yote na kuangalia yale ambayo yanawaumiza wakulima.