Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aleksia Asia Kamguna
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga uzio katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro?
Supplementary Question 1
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Hata hivyo, Mkoa wa Morogoro katika hospitali ya rufaa kuna matatizo ya majengo. Pale ndani majengo yake yako scattered. Sasa inakuwa ni vigumu sana kutoa huduma kwa wakati mmoja.
Je, Serikali imejipangaje kujenga jengo la kuinuka juu (ghorofa) ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wake? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; katika Kituo cha Afya cha Ifakara, kuna matatizo ya kpimo ambacho kinaitwa fetal monitors ambacho kinahusika kwa ajili ya wanawake.
Je, Serikali imejipangaje kupeleka vifaa hivyo ili wale akinamama waweze kupata huduma stahiki? Ahsante.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mazuri ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, suala la kwamba majengo yako mbalimbali (scattered), lakini pia eneo la Hospitali ya Morogoro ni dogo kwa maana ya ukubwa wa eneo lile. Mheshimiwa Waziri wa Afya amekwishaelekeza kwamba, Hospitali zote za Mikoa, Kanda na Taifa wasijenge tena bila kuwa na plan ya hospitali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hospitali zote zimeelekezwa kuchora na kuhakikisha wanakuwa na plan ya ujenzi ambayo inatatua matatizo aliyoyasema na wataleta plan na majengo ya ghorofa yatakwenda juu na sasa ndiyo yatakuwa yanajengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Mheshimiwa Mbunge swali la la Kituo cha Afya, naomba aje sasa hivi kwa sababu Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama alivyoona pale Dar es Salaam alipozindua vifaa mbalimbali, tuwasiliane na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, tuone kifaa hicho, halafu aandike mara moja na aweze kupelekewa kifaa hicho kwenye eneo husika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved