Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza: - Je, lini Serikali itahakikisha mfumo wa uuzaji wa zao la Kakao unaomnufaisha mkulima badala ya wafanyabiashara wachache?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa Serikali ndiyo wanaondesha mfumo huu kupitia vyama vya ushirika, na hapo awali kabla ya kuanza mfumo huu bei ya kakao ilikuwa ni shilingi 7,000 kwa kilo tukiuza kwenye kampuni za botanical; na sasa hivi mfumo huu umeingia wizi mkubwa sana ambao unaendelea mpaka sasa. Kwa sasa zao hili halimnufaishi mkulima wa Kyela mpaka Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa comrade Homera amekiri wazi kwamba mfumo huu unawanufaisha watu wachache na hela haionyeshi kwamba inaingia kwa wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo huu una matatizo sana, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa nini Serikali inaendelea kung’ang’ania mfumo huu ambao haumnufaishi mkulima?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tarehe 7 mwezi wa nane, mwaka 2022 Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara alikiri wazi kwamba mfumo huu utaondoka kwenye zao hili. Je, ni lini sasa Waziri ataenda kuwaambia wananchi wa Kyela kwamba sasa mfumo ambao utamnufaisha mkulima ni huu ambao na wao watakuwa wameujadili naye? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jambo la kwanza namuondoa hofu Mheshimiwa Mbunge, na ndiyo maana mnaona katika matumizi ya huu mfumo tunavozungumza sasa bei ya zao la kakao kwa kilo imefika shilingi 8,000 kwa hiyo unaona kuna maendeleo makubwa. Bahati nzuri katika mfumo huu mkulima analipwa ndani ya masaa 48 baada ya mnada kuwa umekamilika; kwa hiyo utaona kuna manufaa mengi kwenye huu mfumo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Wizara ya Kilimo kwa sababu tunaendelea kupitia hii mifumo na kuangalia kama kuna changamoto basi tunapokea sehemu ya maoni ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyatoa na tutayapitia tuone kama kuna mahali kuna changamoto ili tuweze kuirekebisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kueleza kwamba, ni lini mfumo huu utaondoka nafikiri baada ya mapitio ya changamoto tujue kama kweli kuna changamoto lakini jukumu letu sisi ni kuboresha na kuhakikisha mfumo huu unawasaidia wakulima nchini, ahsante.
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza: - Je, lini Serikali itahakikisha mfumo wa uuzaji wa zao la Kakao unaomnufaisha mkulima badala ya wafanyabiashara wachache?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri alishatoa taarifa kwa Umma kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imeshatoa fedha zote kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa zao la mahindi kule Ludewa. Je, nini maelekezo ya Serikali kwa watu wa NFRA kuwahisha malipo hayo ili wazazi waweze kupeleka watoto vyuo na kununua mbolea? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Bahati nzuri Mheshimiwa Mbunge ameeleza kwamba tuko katika hatua za mwisho kumalizia malipo kwa watu ambao wapo katika awamu ya mwisho. Kwa maelezo ambayo Mheshimiwa Waziri wa Kilimo alikuwa amenipatia, ni kwamba baada ya kumaliza huu mchakato, Serikali itarudi kwa ajili ya kuendelea kununua mazao kwa wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo ni kwamba, kwa sababu fedha hizi ziko katika Taasisi za Kibenki, wanamalizia tu huu mchakato na naamini kabla ya mwisho wa mwezi huu wakulima wote nchini watakuwa wameshalipwa. Ahsante.
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza: - Je, lini Serikali itahakikisha mfumo wa uuzaji wa zao la Kakao unaomnufaisha mkulima badala ya wafanyabiashara wachache?
Supplementary Question 3
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Licha ya mkakati wa Serikali kuruhusu minada ya kahawa, Mkoani Kagera, bado changamoto ya bei inabaki kuwa chini ukilinganisha za majirani zetu wa Uganda, hivyo kupelekea watu kutamani kuvusha kahawa. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha bei ya kahawa Mkoani Kagera haitofautiani sana na Uganda ili watu waweze kupata faida ya kahawa zao?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Swali la namna hii nilijibu nafikiri ndani ya siku mbili au tatu zilizopita, tukaainisha moja ya mchakato wa Serikali wa kuongeza thamani katika zao la kahawa ambao utachangia ongezeko la bei kwa sababu asilimia kubwa ya kahawa ambayo tunauza sisi ni kahawa ghafi ambayo inapelekea bei kuwa chini. Nimthibitishie kwamba mkakati wetu juu ya uwekezaji katika zao la kahawa uko palepale na tutawasaidia wakulima katika maeneo yote nchini wanayolima ikiwemo katika Mkoa wa Kagera. Kwa hiyo nimwondoe shaka Mbunge katika hili, hii kazi tunaiweza na tutaifanya. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved