Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 1

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, naishukuru Serikali kwa kutenga fedha lakini tangu mwezi wa saba mpaka leo fedha hiyo haijapelekwa.

Je, ni nini kauli ya Serikali katika kuhakikisha kwamba fedha hiyo inapelekwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali inasema nini katika kuongeza mawanda ya utoaji elimu ili kuinusuru jamii na tatizo kubwa la magonjwa haya ambavyo yameendelea kuongezeka?
Ninalisema hilo kwa sababu, kwa sasa hivi ili jamii tuepuke suala la kwenda kwenye tiba, Serikali inasema nini kwa maana ya elimu ya kinga? Nakushukuru (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Kapufi, kwa kweli amekuwa akifuatilia hospitali ile na mimi na yeye tumeshakwenda zaidi ya mara nne kwenye Hospitali ya Mkoa wa Katavi. Nimwambie tu, kabla ya mwezi wa pili kuisha, fedha zitakuwa zimefika kwenye Hospitali yenu ya Mkoa wa Katavi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenykiti, swali lake la pili ni suala la magonjwa yasiyoambukiza kuongezeka, na kila mwaka matatizo hayo yanaongezeaka kwa asilimia 10. Ni kweli tunahitaji mkakati na tunaendelea. Nimuombe kila mtu tuweze kufanya hizo hamasa na zinaendelea. Tumeshaanzisha vipindi kwenye redio na kupitia makongamano mbalimbali. Nawaomba Wabunge, kile kipindi anachokiendesha Profesa Janabi, ninawaomba huo ni mkakati muhimu sana. Kwa hiyo, anachokisema Profesa Janabi naomba usikipuuze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo ukwali halisi na hicho kipindi hakiko kwa bahati mbaya. Profesa Janabi anaendesha kwa ajili ya kutunusuru na ni mkakati maalumu wa Wizara na Hospitali yenu ya Taifa ya Muhimbili ambayo ndiyo yenyewe inabeba mizigo mikubwa kutokana na hayo magonjwa. (Makofi)

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu haina wodi za kulaza wagonjwa.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kujenga wodi hizo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakishia tu Mbunge, kwenye hizi hospitali zote ambazo ni mpya ambazo ziko kwenye utaratibu wa kuedelea kujengwa, zimetengewa fedha ikiwemo Hospitali yake ya Simiyu. Kabla ya mwezi Februari kwisha, fedha zitakuwa zimefika ili kuendeleza ujenzi huo ambao ulitakiwa kumalizika. (Makofi)

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 3

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niulize swali fupi la nyongeza. Kituo cha Afya cha Uru Kusini tayari kimekamilika lakini hakuna madaktari. Ni lini Serikali itapeleka madakatari katika kituo hiki cha afya ili Wananchi wa Uru Kusini waweze kuhudumiwa? Ahsante sana.

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kweli hicho kituo kiko namna hiyo. Cha kwanza, leo leo nikienda kukaa kwenye kiti nitaongea na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro ili kuona ni namna gani tunaweza ku-switch watendaji ndani ya mkoa au ndani ya wilaya, kupeleka kwenye eneo hili wakati tunashirikiana na wenzentu wa TAMISEMI kuhakikisha wanapatikana watumishi wa kwenda kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 4

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, kwa kuwa gharama kubwa ya usafishaji wa figo hailingani na mapato ya Mtanzania wa ngazi ya chini au wa kipato cha chini; je, Serikali ina mpango gani sasa wa kusaidia kupunguza gharama ya usafishaji wa figo kwa wagonjwa? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka utaratibu mzuri sana wa kuwahudumiwa wale wasio na uwezo wa kupata tiba. Kwa hiyo, kwa wale ambao hawana uwezo wa kujigharamia, kuna utaratibu wa kufuata. Pia kwa kweli ameuliza swali zuri na linagusa watu wengi. Namwomba Mheshimiwa Mbunge kwamba yeye na mimi na wengine tunakwenda kuanza mchakato wa Bima ya Afya kwa Wote. Hiyo ndiyo itakuwa suluhisho kwa wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnakumbuka, juzi niliulizwa swali hapa. Ikaonesha kuna tiba ukiziacha tu zikaenda bure, huduma nyingine kwenye nchi zina-collapse. Kwa hiyo, twendelee kushirikiana kwa sababu, hata bei wanazolipa sasa hivi, watu bado wanachangia kwenye huduma hizo.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 5

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa magonjwa ya ini yamekuwa ni tishio hapa nchini, na gharama ya kupata chanjo ni kubwa kwa wananchi wetu ambao hawana uwezo, wa kipato cha hali ya chini; je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kutoa chanjo hiyo kwa wananchi wote kama chanjo zingine?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimmiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge, tumeanza mchakato huo na muda si mrefu utakamilika kwa ajili ya kuona namna ya kutekeleza wazo zuri ambalo Mheshimiwa Mbunge unasema. Tayari tumeshaanza namna ya kuunganisha na chanjo nyingine; ionekane bajeti inapatikanaje ili kuweza kutoa hiyo huduma chanjo nyingine zinavyotolewa.

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 6

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru; magonjwa ya figo yamezidi kuongezeka katika Mkoa wetu wa Tabora.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete ili kuwaondolea wananchi usumbufu na gharama kubwa wanazozipata katika hospitali binafsi? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge. Kwanza huduma hizo zipo kwenye Hospitali ya Kitete lakini haziko strong kuweza kutatua matatizo tuliyonayo, hasa makubwa yanayohitaji special attention. Kwa hiyo, kwa mwaka huu ndiyo hospitali tunazoendelea kujenga. Vifaa kwa ajili ya Hospitali yako ya Kitete kwa ajili ya masuala ya figo vimeshafika. Tunamalizia ukarabati wa baadhi ya maeneo ili hiyo shughuli iweze kuanza. (Makofi)

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: - Je, ni lini jengo la huduma ya usafishaji damu kwa wagonjwa wa figo litajengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi?

Supplementary Question 7

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa gharama za matibabu ya figo watu wanapoenda kusafisha damu ni kubwa sana, takribani shilingi 540,000 kwa wiki; na kwa maana hiyo ni takribani shilingi 2,160,000 kwa mwezi, gharama ambazo ukweli ni kwamba wananchi wetu wanashindwa ku-afford na wengi wanapoteza maisha. Sasa haya mambo mengine ya bima tunajiandaa na bima na nini na Bunge hili lilishawahi kutoa msamaha mwingi katika maeneo mengi, kwa nini wagonjwa hawa wasitibiwe bure na tukatoa msamaha katika hili eneo na tukafidia kwa ajili ya maeneo mengine? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia Mheshimiwa Mbunge, kwa kweli wazo lake lina nia njema, lakini nataka kuwaambia, juzi hapa tumeonesha kuna zaidi ya shilingi bilioni 70.4 zimesamehewa kwenye eneo hilo ambalo Mheshimiwa analisemea. Tutaendelea kuchakata, kwa sababu sasa hivi tunaenda kwenye michakato ya bajeti na vitu vingine, watupe muda tuone. Kwa sababu, tunaweza kuahidi hapa, tukaahidi na isiweze kutekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Afya ameshafanya kazi kubwa sana ya kukaa chini na wataalamu wetu. Hizi huduma za figo zinaenda kushuka sana kwa sababu tumeshapata watu wanaoweza kutoa madawa na vile vifaa vinavyotakiwa kutoa huduma hiyo kwa bei rahisi zaidi na huduma hizo zitaenda kushuka sana. Haitakuwa kama bei aliyokuwa anaisema Mheshimiwa Mpina hapo.