Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Nambalapi, Kata ya Masunya – Tunduru utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu ya Umwagiliaji ya Nangalapi kuna bwawa na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umefanyika kwa maana ya mifereji na banio; je, upi mpango wa Serikali wa kuunganisha wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwenye bwawa ili kuweza kuunganisha mradi ule uweze kufanya kazi kwa pamoja na kuongeza tija ya maji?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimuondoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba usanifu wa kina uliofanyika ni complete package ni mradi wote mzima ikiwemo katika hayo maeneo ya banio ambayo Mheshimiwa Mbunge ameeleza pamoja na bwawa. Kwa hiyo, utakapo kwenda kujengwa utajengwa kama mradi mzima kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote.
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Nambalapi, Kata ya Masunya – Tunduru utaanza?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, nataka kujua ni lini Serikali itatumia ipasavyo rasilimali maji iliyopo Ukerewe kukamilisha na kuimarisha miradi ya umwagiliaji iliyopo Ukerewe?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Ukerewe ni miongoni mwa halmashauri ambazo zipo katika mpango wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ajili ya kujengea miradi ya umwagiliaji. Kwa hiyo, tunachokifanya sasa hivi katika bajeti tunapeleka katika kila eneo kulingana na mahitaji. Kwa hiyo, tutafikia maeneo yote ikiwemo eneo la Ukerewe.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Nambalapi, Kata ya Masunya – Tunduru utaanza?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nianze kwa kumshukuru sana Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji kwa kutembelea skimu za umwagiliaji kwenye Jimbo la Vunjo; swali langu ni lini sasa wataanza ukarabati wa skimu ya mfereji ile ambayo ipo kule kwenye Kata za Mwika Kaskazini, Mwika Kusini, Mamba Kaskazini na Kusini na Marangu, Kilema na Kirua Vunjo?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, katika Jimbo la Vunjo tunatambua kazi nzuri ambayo imeendelea kufanyika kule na baadhi ya skimu zipo katika mipango yetu inayokuja. Mingine tunaendelea na upembuzi yakinifu na mingine tunatafuta fedha ili tuanze usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi. Kwa hiyo, kila skimu ambazo zipo zipo katika kila hatua, kwa hiyo, tutampa taarifa Mheshimiwa Mbunge mradi gani utaanza lini na upi utafuatia.
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Nambalapi, Kata ya Masunya – Tunduru utaanza?
Supplementary Question 4
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi, kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024 Mbungi Vijijini tulipangiwa kujengewa mabwawa mawili. Bwawa la Mungahai na Bwawa Diri; je, lini mnajenga mabwawa haya?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mabwawa yaliyopo Mbulu Vijijini yapo katika mpango wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa ajili ya utekelezaji wake. Ambacho kinafanyika sasa hivi ni ule upembuzi na usanifu wa kina. Tukishamaliza hapo maana yake tutakwenda katika hatua ya pili ya kuanza ujenzi.
Name
Kiswaga Boniventura Destery
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Primary Question
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Kijiji cha Nambalapi, Kata ya Masunya – Tunduru utaanza?
Supplementary Question 5
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, Skimu ya Magubike katika Kata ya Nzihi iliahidiwa tangu mwaka 2007 na Serikali imekuwa ikifuatilia ikaahidi kwamba itakuja kujenga. Sasa itakuja kujenga lini maana bado tunasubiri?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Skimu ya Magubike iliyopo Kalenga na yenyewe ipo katika mipango ya Tume ya usanifu wake wa ujenzi na upembuzi yakinifu. Tukishamaliza hiyo hatua maana yake hatua ya pili ni kumtafuta mkandarasi, baada ya hapo tutaingia katika hatua ya mwisho kwa ajili ya ujenzi. Kwa hiyo, nimuondoe shaka Mheshimiwa Mbunge. Jambo hilo tunalifahamu na lipo katika bajeti zetu.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved