Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza eneo la ekari 1,000 lililotengwa kwa matumizi ya viwanda Kata ya Pembamnazi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali lingine la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, eneo hili lilipimwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na mahitaji ya ardhi kwa uwekezaji katika Wilaya ya Kigamboni ni kubwa sana.

Je, ni ipi mikakati ya Serikali ya kulitangaza eneo hili kwa ajili ya uwekezaji?

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kushukuru na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake anazofanya katika kukuza uwekezaji na tumeanza kupata maombi ya uwekezaji katika eneo hili. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge na yeye kwa kutumia influence yake na Bunge lako Tukufu kuendelea kuwatangazia wawekezaji wote wenye nia ya kujenga viwanda kuweza kuwasilisha maombi yao. Ahsante.

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza eneo la ekari 1,000 lililotengwa kwa matumizi ya viwanda Kata ya Pembamnazi?

Supplementary Question 2

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Je, ni ipi kauli ya Wizara ya Ardhi kuwasaidia wananchi ambao maeneo yote yaliyokuwa yametengwa ya kutumika ya umma yakaporwa na watu ambao wanajiita ni wawekezaji; kwa mfano, Kijiji cha Msungwe, ata ya Kapele yuko mwekezaji ambaye amepora ardhi ya kijiji yenye zaidi ya ekari 1000; ni upi msaada kutoka kwenye Wizara hii?

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, maeneo ya ardhi za vijiji kikiwemo Kijiji cha Msungwe kwenye Jimbo la Momba yanaongozwa na Sheria Na. 5 ya Ardhi ya mwaka 1999 ambayo inatoa mamlaka ya wananchi kusimamia ardhi yao na kutoa kiasi cha ardhi kinachogaiwa kwenye kila ngazi kutoka kijiji, wilaya na mpaka Kamati ya Uwekezaji ya Taifa. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge awasilishe malalamiko ya wananchi wao na tutaishughulikia na tutatoa majibu na haki ya wananchi itapatikana. (Makofi)