Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. David Mathayo David

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Same Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. DAVID M. DAVID K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Je, ni tafiti ngapi za mafuta zimefanyika nchini na yapi matokeo ya tafiti hizo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza hapa. Kwanza, ningependa kujua katika maeneo haya ambayo yanafanya utafiti wa gesi na mafuta ni leseni ngapi zimetolewa kwa ajili ya uchimbaji wa gesi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, napenda kujua Serikali ina mkakati gani wa kuendelea kunadi vitalu hivi ili kupanua wigo wa uwekezaji na kuweza kuthibitisha zaidi kiasi cha rasilimali hizi ambazo tunazo nchini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hadi sasa kwa maeneo haya 84 ambayo tunafanya tafiti, tunazo jumla ya leseni 11 ambapo leseni nane ni za utafutaji na leseni tatu ni za uzalisahaji wa gesi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, kwa sasa hivi Wakala wa Udhibiti wa Mkondo wa Juu Wa Petroli (PURA) akishirikiana na Wizara tunao mkakati wa kuendelea kufanya maandalizi ya kunadi zabuni za vitalu kwa ajili ya kuleta wawekezaji zaidi ili kufanya tafiti na kuthibitisha rasilimali hii, ahsante.