Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, ni kuna mpango gani wa kukarabati skimu ya umwagiliaji ya Masengwa-Shinyanga?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri. Kwa kuwa katika majibu yake amesema kwamba ni hekta 133 tu ambazo zinamwagiliwa na kuna hekta 407 ambazo zimebaki; je, ni lini hiyo kazi ya kuhakiki itaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Eneo la Mwamnyepe, Kata ya Bubali kuna mto na kuna umwagiliaji ambao wananchi wao wenyewe walianzisha; je, ni lini Serikali itakwenda kukarabati na kuboresha mradi wa umwagiliaji ambao umeanzishwa na Wananchi wa Bubali? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba tumeweka commitment ya Serikali kwenye Mradi wa Umwagiliaji Masengwa ambao uhakiki unaendelea sasa hivi na tutamaliza katika mwaka huu wa fedha; na ndiyo maana commitment yetu katika mwaka wa fedha unaokuja 2024/2025 tutaingiza katika bajeti yetu ili utekelezaji uanze.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kata ya mradi ambao umeanzishwa na wananchi jambo hilo na lenyewe tumelipokea ninaiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji iende ikafanye uhakiki ili sasa tutafute fedha kwa ajili ya kuweka kwenye bajeti. (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, ni kuna mpango gani wa kukarabati skimu ya umwagiliaji ya Masengwa-Shinyanga?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa hii nafasi, Skimu ya Umwagiliaji ya Msenembo iliyopo katika Halmashauri ya Manyoni ina hali mbaya sana. Mwaka huu wakulima wameshidwa kulima kabisa. Je, Serikali ina mkakati upi wa kuwanusuru wakulima hawa ili waweze kuendelea na kilimo chao cha umwagiliaji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali kwenye skimu zote, na ndiyo malengo ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametuelekeza; moja, kuhakikisha tunaekebisha skimu zote ambazo zilikuwa zinatumika awali na sasa hivi zinahitaji marekebisho makubwa.

Pili, kuhakikisha maeneo yote yanayofaa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji tunajenga miradi mipya kwa ajili ya umwagiliaji. Tatu tujenge mabwawa makubwa ya umwagiliaji ili kuhakikisha wananchi wanalima katika kipindi chote cha msimu yaani kwa maana ya mwaka mzima. Kwa hiyo mkakati uliopo kwako upo katika maeneo yote. Niwahakikishe wananchi kwamba Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na uhakiki katika maeneo yote nchini.

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, ni kuna mpango gani wa kukarabati skimu ya umwagiliaji ya Masengwa-Shinyanga?

Supplementary Question 3

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri mwaka juzi na mwaka jana mmeahidi kupeleka fedha kwenye Skimu ya Ruafi, lakini mwaka huu hali ni mbaya na wakulima hawawezi kuendelea kulima. Je, mna mkakati gani sasa kupeleka pesa kwa haraka na mkarabati ile skimu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Skimu ya Ruafi na yenyewe ni moja ya skimu ambayo tume yetu imepata taarifa juu ya kinachoendelea kule na sisi Waziri wa Fedha amekutana na Waziri wa Kilimo kuhakikisha wanatupatia bajeti ili yale maeneo yote ambayo yameharibika sasa tuweze kuyarekebisha. Kwa hiyo hili nikuondoe shaka na tunalifanyia kazi.