Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Venant Daud Protas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isitoe elimu pamoja na chanjo bure kwa wafugaji wa ng’ombe nchini?

Supplementary Question 1

MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza; tumekuwa na chanjo nyingi ambazo sisi kama Serikali tunapeleka. Tumepeleka chanjo za surua tunatoa bure. Tumepeleka pepopunda tunatoa bure. Ni kwa nini sasa, Serikali isipeleke chanjo za mifugo na zikatolewa bure na wataalam wetu wakatumika kutoa hizo chanjo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; tumekuwa na chanjo ambazo zinaendelea katika halmashauri zetu na majimbo yetu, lakini hizi chanjo zinatolewa tender na wazabuni wana-tender wanakwenda kuchanja kule, lakini mfugaji akipata athari kwenye mifugo yake hakuna msaada wowote ambao anaweza kuupata kupitia hao watoa huduma. Je, Serikali haioni haja ya kupeleka madawa na wataalam wetu wakaenda kuwachanjia wafugaji wetu ili ziweze kuwasaidia direct na wakipata matatizo wajue wapi wanakwenda? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba, chanjo nyingi zimekuwa zikitolewa bure, chanjo za binadamu na maeneo mengine. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba Mwaka wa Fedha 2024/2025, tayari Serikali imekwishatenga bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 29, kuanza kutoa chanjo bure kwa mifugo yetu ambayo wananchi wetu wanamiliki katika maeneo yao. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mwaka huu katika bajeti hii itakapokuja aipitishe kwa kishindo ili twende kutekeleza jambo hili ambalo na yeye yamekuwa ni maono yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili tumepokea ushauri na ushauri huu tutakwenda kuufanyia kazi tuone namna ambavyo Serikali kupitia Wizara inaweza kuutekeleza ushauri huu. Ahsante. (Makofi)

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isitoe elimu pamoja na chanjo bure kwa wafugaji wa ng’ombe nchini?

Supplementary Question 2

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Katika Kata ya Mkindi kuna Kijiji cha Kihwenda ambapo panajengwa bwawa kwa ajili ya wafugaji. Ni takribani mwaka wa pili sasa Mkandarasi ameondoka site na bwawa lile ni muhimu sana kwa maji kwa ajili ya wafugaji pamoja na wananchi. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kuwa, Mkandarasi anarudi na bwawa lile linakamilika? Ahsante. (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli bwawa hilo limesimamishwa ujenzi wake. Nimhakikishie Mbunge tutakwenda kufuatilia, tutaangalia mimi na yeye twende kule, tuangalie na wataalam tuone namna ambavyo tunamrudisha Mkandarasi site ili aweze kukamilisha bwawa hilo na wananchi waweze kupata huduma katika eneo hilo. Ahsante. (Makofi)