Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rose Cyprian Tweve
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: - Je, nini mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa zao la pareto?
Supplementary Question 1
MHE. ROSE C. TWEVE: Mheshimiwa Spika, zao la pareto ni zao ambalo tuna uhakika na soko duniani. Wilaya ya Mufindi tuna kiwanda kikubwa cha pareto ambacho kina uwezo wa kuchakata tani 10,000 kwa mwaka lakini mpaka sasa hivi wanachakata tani 2,400 tu.
Swali langu kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha hizi program kama za BBT ziweze kufika Mufindi, kwa sababu kitu kinachotakiwa pale ni eneo na vijana wa kufanya kazi hizo tayari wapo ili kuhakikisha tuna-feed kile kiwanda ili kiweze kuzalisha kwa uwezo ambao kiliwekwa pale? (Makofi)
Swali la Pili; sasa hivi zao la pareto limewekwa kwenye Bodi ya Mazao Mchanganyiko, kwa unyeti wa zao hili, Je, huoni zao hili sasa liwekwe kwenye bodi pekee ambayo italimamia ili zao hili liwe na tija? Nakushukuru sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na sisi kama Wizara tunatambua kwamba tunazalisha pareto kwa kiwango cha chini na tunahitaji mikakati ya ziada ikiwemo kutumia kwenye programu zetu za BBT kuongeza uzalishaji wa zao la pareto.
Mheshimiwa Spika, Wizara jambo hili tumelipokea na tutalifanyia kazi hususan katika Eneo la Mafinga ili tuweze kuongeza tija katika zao hili na ambalo litasaidia katika vile viwanda ambavyo vinachakata pareto. Kwa hiyo hilo tumelipokea.
Mheshimiwa Spika, kuhusu zao la pareto kupelekwa kwenye Bodi ya Mazao Mchanganyiko, ni kwamba sasa hivi liko kwenye mamlaka ambayo inaitwa COPRA ndiko ambako inaelekezwa, sababu kubwa ni kwamba awali kulikuwa na Bodi inayojitegemea na ilionekana haifanyi vizuri ikiwemo masuala ya resources na mambo ya kiutawala, kwa hiyo imepelekwa kule kwa lengo la kuongeza tija ili tuweze kuisaidia. Pamoja na yote bado Serikali inaweza kupitia mchakato na kuangalia namna bora ya kutoka hapa ambapo tulipo, ahsante. (Makofi)
Name
Cosato David Chumi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: - Je, nini mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa zao la pareto?
Supplementary Question 2
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kama ambavyo imeelezwa katika swali la msingi, zao hili ni muhimu sana. Sasa ili kiwanda kipate malighafi kwa maana ya maua, kiwanda kile kiko kwenye mazungumzo na Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Magereza ili kukodi eneo katika Gereza la Isupilo ili waweze kuzalisha maua kama sehemu ya malighafi.
Je, Wizara ya Kilimo iko tayari kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani kuhakikisha kwamba mpango huo unakuwa fast trucked ili eneo hilo lipatikane kwa wakati? (Makofi)

Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Wizara ya Kilimo kwenye jambo lolote jema na lenye tija ya kuongeza uzalishaji kwenye zao la pareto, tuko tayari kushirikiana na Wizara yoyote ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Magereza ili kuhakikisha tunapata eneo na kuongeza uzalishaji katika zao la pareto, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved