Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji za Katengera, Muhwazi, Gwanumbu na Ruhwiti katika Wilaya ya Kakonko zitakarabatiwa?

Supplementary Question 1

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, moja, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Katika majibu ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ametoa, ameunganisha skimu mpya zinazotarajiwa kuanzishwa na skimu ambazo zipo sasa.

Mheshimiwa Spika, hoja yangu kubwa ni kwamba, Skimu ya Murwazi, Ruhwiti na Katengera zipo. Tatizo ni miundombinu yake imeharibika na hivyo hazifanyi kazi inavyostahili. Swali langu, ni lini Serikali itapeleka fedha hizo kwa haraka ili kuhakikisha skimu hizo zinakarabatiwa na ujenzi unafanyika ili wananchi waweze kufaidi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa baada kikao hiki twende pamoja ili kuhakikisha kwamba anaiona skimu hizi ili kutoa suluhisho haraka sana? Ahsante sana.

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, moja ya maelekezo ambayo tumeyapata kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha kwanza tunakarabati skimu zote ambazo zilikuwepo na zimeharibika. Pili, tujenge maeneo mapya na kutambua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hayo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, sasa katika maelekezo yake, sasa hivi tunapotaka kufanya maboresho ya hizi skimu zilizoharibika, ni lazima tufanye upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili tupate gharama halisi, tofauti na ule utaratibu uliokuwa unatumika zamani, mtu akiona tu dharura anapeleka shilingi milioni 500, lakini hajui kuna gharama kiasi gani zinahitajika. Ndiyo maana kulikuwa na mwendelezo wa matatizo mengi katika skimu zetu nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hilo kwa sasa hivi lipo katika utekelezaji na tukimaliza tu tutatenga fedha kwa ajili ya kuzikarabati na kuzijenga. Kuhusu kwenda, niko tayari mara tu baada ya Bunge lako Tukufu kumalizika.

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, lini Skimu za Umwagiliaji za Katengera, Muhwazi, Gwanumbu na Ruhwiti katika Wilaya ya Kakonko zitakarabatiwa?

Supplementary Question 2

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi; je, ni lini Serikali itampata mkandarasi katika Jimbo la Singida Kaskazini kwenye Skimu ya Umwagiliaji Msange.

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Isange, nafikiri Tume ya Umwagiliaji ipo katika mchakato. Pia, mnafahamu kwamba mchakato ni hatua, ukishakamilika tu maana yake tutatangaza mkandarasi ambaye anahusika katika ujenzi wa Skimu ya Msange, ahsante.