Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ali Juma Mohamed
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. ALI JUMA MOHAMED K.n.y. MHE. MAULID SALEH ALI aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti mfumo wa makosa ya kimtandao (cyber crime) ili yasitokee nchini?
Supplementary Question 1
MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina ushauri mdogo tu kwa Serikali. Kwa vile haya makosa ya uhalifu mitandaoni yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, ninaishauri Serikali ijaribu kukiwezesha Kitengo hiki cha Cyber, ili kiwe na mfumo mzuri wa kufanya kazi zake kwa wepesi pamoja na kujaribu kurekebisha baadhi ya sheria ambazo zimekuwa kikwazo katika utendaji wao wa kazi za kila siku.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri na tutaufanyia kazi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved