Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 1
MHE. FATMA H. TAUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa reli hii ni muhimu sana kwa uchumi wa ukanda wa Kusini Magharibi na pia ni muhimu sana kwa usafirishaji mizigo kwa nchi jirani za Kongo, Burundi na Rwanda: Je, Serikali haioni sasa imefikia wakati kuharakisha kujenga reli hii ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata tija? (Makofi)
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Taufiq, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Serikali inatambua umuhimu wa reli hii na inatambua kwamba nchi jirani kama Kongo, Zambia ni wadau wetu na ndiyo tunaofanya nao kazi na mizigo mingi inatoka katika hizo nchi. Kwa maana hiyo, Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka wa fedha ujao wa 2022/2023 imetenga kiasi cha Shilingi 199.4 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hii.
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 2
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kukamilika kwa barabara ya kutoka Tabora kwenda Mpanda na kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Karema ni kishawishi kikubwa sana cha nchi jirani ya DRC Congo kutumia huduma ya bandari ile, na wameshaanza kuleta hiyo huduma:-
Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wa haraka zaidi kukamilisha kile kipande cha ujenzi wa reli kutoka Mpanda kwenda Karema ili kiweze kuwa kiunganishi na nchi jirani?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kakoso kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba kwanza tumejenga hiyo bandari ya Karema na upande wa pili ni Karemii kwa wenzetu Congo na Wizara kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kukamilisha kipande hiki cha Mpanda – Karema. Ndiyo maana tumetenga kiasi hiki cha fedha kiasi cha Shilingi 199.4 ili iwe na tija hiyo barabara na bandari yetu ambayo tumejenga ya Karema.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Name
Sebastian Simon Kapufi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Mjini
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 3
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ujenzi wa Treni hauwezi ukaacha mbali ujenzi wa vituo vya reli, kituo cha reli cha Mpanda ni chakavu, Waziri anasema nini katika kuhakikisha kituo kile kinajengwa?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sebastian Kapufi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli tunatambua kipande hiki cha kutoka Kaliua – Mpanda kina changamoto ya miundombinu pamoja na station. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika bajeti ambayo Bunge imetuidhinishia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia TRC, Shirika letu la Reli Nchini, tumetenga kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa station iliyopo pale Mpanda Mjini pamoja na kuboresha miundombinu mingine katika Reli hii ya Mpanda – Karema. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 4
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Ahsante sana. Kuna treni ya TAZARA ambayo inatoka Dar es Salaam mpaka Tunduma. Je, upi mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba inaipanua treni hiyo ili iwe ya mwendokasi na iweze kukidhi mahitaji ya nchi yetu kwa Nyanda za Juu Kusini? (Makofi)
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Japhet Hasunga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba reli yetu ya TAZARA inaongozwa na nchi mbili kati ya Tanzania na Zambia. Kumekuwepo na changamoto nyingi katika uendeshaji wa reli hii, lakini habari njema ni kwamba ndani ya mwezi huu ifikapo tarehe 30 ya mwezi huu Mawaziri wa pande zote mbili kutoka Tanzania na Zambia watakutana. Lakini pili, tunataka tubadilishe Sheria. Hivi sasa Sheria inayotumika ni Sheria ya tangu ilivyoanzishwa TAZARA. Sasa sisi upande wa Tanzania tukitaka tuwekeze tunashindwa kwa sababu ile Sheria imetubana. Tayari maandiko au maandalizi ya Sheria hii imeshapitishwa. Kwa hiyo tunasubiri sasa kikao hicho cha Mawaziri watakapokaa halafu hizo Sheria zije ndani ya Bunge la Tanzania za upenda wa Zambia ili tuweze kuhuisha hii reli. Ahsante. (Makofi)
Name
Tunza Issa Malapo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 5
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nataka kujua Serikali imefikia hatua gani katika ujenzi wa reli ya kutoka Mtwara mpaka Bambabeyi? Ahsante.
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Ningependa kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Malapo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli reli yetu ya kutoka Mtwara kuja Bamba Bay pamoja na matawi mawili ya Liganda na Mchuchuma imetengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 100, lakini pia tumepata ufadhili wa SADC kiasi cha dola za Kimarekani milioni sita. Na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina tayari umekwishafanyika katika reli hii. Ahsante.
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 6
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha treni inayotoka stesheni kwenda Pugu inayojulikana kwa jina la treni ya Mwakyembe kwa kuweka miundombinu ya vituo ili kuepusha ajali zinazojitokeza baina ya treni na magari?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli treni hizi ambazo zinatusaidia sana Mji wa Dar es Salaam, hususan kipindi cha asubuhi na jioni ambacho kunakuwa na foleni kubwa kuna changamoto baadhi ya maeneo. Sisi upande wa Shirika, kupitia Shirika letu la reli nchini tumejipanga kuboresha maeneo yote hususan maeneo yale ya makutano kati ya barabara na treni ili kuweka alama. Na alama hizi zitaenda na elimu pia kwa jamii katika mazingira hayo kwa sababu wakati mwingine treni inapopita kunakuwa na changamoto pia ya watu kupita na huwa zinatokea hizo ajali. Kwa hiyo tumejipanga kutoa hiyo elimu, lakini tutaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya Dola hususan Polisi kwa ajili ya kuelimisha jamii katika maeneo hayo ambapo kuna makutano kati ya barabara na reli. Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 7
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza kabisa naishukuru Serikali na baada ya kuishukuru Serikali, nauliza kuwa ni lini reli ya Mwendokasi kuanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro itaanza kazi, tegemeo la Serikali? Ahsante.
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza nitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha takribani zaidi ya trioni 6.5 kwa Wakandarasi wote katika Standard Gauge. Lakini pia tumeingia Mikataba zaidi ya dola la Kimarekani bilioni 7.2, takribani trioni 15 pamoja na VAT. Sasa reli hii ya kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro yenye urefu wa kilomita 300 tunategemea itaanza rasmi mwezi wa tisa, operation zake zote zitaana mwezi wa tisa. Na mwezi wa Nane yataingia yale mabehewa pamoja na vichwa; kwa sababu sasa hivi tunachokifanya ni kufanya testing kwa maana ya vituo, stesheni kwa stesheni, umeme, signals na kila kitu ndicho kinachofanyika kwa wakati huu. Ahsante. (Makofi)
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ K.n.y. MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa treni ya mwendokasi kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema?
Supplementary Question 8
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Ninajua kabisa uchumi wa Nyanda za Juu Kusini unategemea pia reli ya TAZARA. Tunajua kwamba kama ulivyosema mnataka kubadilisha Sheria lakini bado mabehewa ni chakavu na wateja ni wengi. Tunajua tukitumia treni hiyo tutasaidia kurahisisha barabara kupona wakapeleka kwenye treni. Ni lini Serikali sasa itawekeza zaidi kwenye kuleta mabehewa mapya na kutengeneza miundombinu vizuri?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu swali la nyongeza kupitia Mheshimiwa Japhet Hasunga, kwamba kilichokuwa kimetubana sana kama nchi ilikuwa ni Mkataba tuliyoingia. Kwa hiyo ulikuwa huwezi kufanya namna yoyote ile hata kama nchi inatoa trioni moja hivi sasa, lakini upande wa pili wasiwekeze chochote automatically hiyo fedha baadaye mtagawana equally. Kwa hiyo mwarobaini wa TAZARA ni hii Sheria ambayo nimesema tarehe 30 Juni, 2022 Mawaziri wetu watakutana na Sheria ile itakuja ili na sisi tuwekeze upande wa Tanzania na wao wawekeze upande mwingine.
Mheshimiwa Spika, lakini zaidi nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge pia kwamba Sheria iliyopo kwa sasa inaruhusu pia wawekezaji binafsi. Kwa hiyo kupitia PPP tunawakaribisha wawekezaji ili tuweze kununua hayo mabehewa. Ahsante. (Makofi)