Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, ni lini Serikali italeta Bungeni mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki ili iwezeshe Mkataba wa Marakesh kutekelezeka kwa mujibu wa Sheria?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo ya nyongeza. Kwanza nianze na kumshukuru Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa ajili ya majibu haya ya Sheria hii ya Marakesh.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Sheria hii inaruhusu Authorized Entity inaweza kuzalisha kazi ya msanii bila idhini yake kwa matumizi ya beneficially person. Je, Serikali imewajulisha wadau juu ya hili?

Swali langu la pili, je, mchakato wa Kanuni unategemea kukamilika lini ili wanufaika hasa watu hawa wenye ulemavu waweze kunufaika na sheria hii? (Makofi)

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, nikushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ritta, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Ritta, kwamba wadau wameshirikishwa wakati wa kuandaa Sheria hii. Lakini kama kutakuwa na uhitaji wa kuendelea kuwashirikisha Wizara yetu iko tayari kuendelea kuwashirikisha.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili, alipenda kufahamu ni lini Kanuni hizi zitakamilika. Kama nilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi, kwamba tarehe 07 Februari, 2022 tulipitisha Sheria hii. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Ritta kwamba Kanuni zipo katika hatua za mwisho zikikamilika wadau pia tutawashirikisha waweze kuzifahamu. Ahsante.