Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; tutakubaliana kwamba ili kilimo kivutie ni pale ambapo kinakuwa na tija kwa maana ya productivity. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba uzalishaji kwa kila hekari inaongezeka ili tulingane na nchi zingine? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa kilimo kinahitaji mtaji na ni ukweli usiopingika kwamba benki yetu ya kilimo haina uwezo kimtaji na kimuundo. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba benki hii inawezeshwa ili iweze kuwafikia wananchi wengi? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja kati ya changamoto kubwa ambayo inawakabili wakulima wa Tanzania ni kulima kwa tija. Serikali katika kutatua changamoto hii hivi sasa inaendelea kuwawezesha Maafisa Ugani kuhakikisha wanawafikia wakulima na kuwapa elimu bora na kanuni bora za kilimo ili wakulima wetu waweze kulima kwa tija sambamba na upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, katika eneo hili pia TARI wameendelea kufanya tafiti mbalimbali kuhakikisha wakulima wetu wanapata elimu bora ili waweze kulima kwa tija na tunayo mifano ambayo imetokea katika Mkoa wa Mwanza, Simiyu na Geita kwenye kilimo cha pamba ambapo kanuni ile ya 9060 imesaidia sana kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la kuhusiana na mitaji, ni dhahiri kwamba kilimo hakiwezi kuendelea pasipo kuwepo na mitaji katika kusaidia kuchochea sekta hii. Yalitoka maelekezo kupitia benki yetu kuu ya kuhakikisha taasisi zote za kifedha ambazo zinatoa mikopo zifikishe riba ya digit moja kwa maana ya tarakimu moja ili wakulima wetu waweze kukopesheka kirahisi. Zoezi hilo limefanyika katika baadhi ya mabenki na mkakati unaendelea kuhakikisha kwamba na benki nyingine zote zinafikia katika hatua hiyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuiwezesha TADB ni dhahiri kwamba Wabunge wote wameshuhudia kazi ambayo imefanywa na Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha kwamba benki hii inapata mtaji wa kutosha na benki hii ilisaini makubaliano na benki kutoka Ufaransa kwa ajili ya kuongeza mtaji. Vilevile, tunaweka nguvu kubwa kuhakikisha kwamba TADB inasimama kwa dhati ili iweze kuwasimamia wakulima wengi ambao wanashindwa kukidhi masharti katika taasisi za kifedha za kibiashara ili wao wabaki kama guarantor na wakulima waweze kukopesheka. (Makofi)

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 2

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naipongeza Serikali kuiongezea Wizara ya Kilimo bajeti yake kwa asilimia 300. Kwa kuwa vijana wa Tanzania sasa wako wengi wenye nguvu lakini hawana namna ya kuwekeza kwenye taasisi kama hiyo sekta ya kilimo; na kwa kuwa kwenye jibu la msingi, Waziri ametueleza kwamba wako tayari sasa kuona kwamba tunajitosheleza kwa chakula. Je, Serikali inawatumiaje vijana hao wengi kwa kuwawezesha katika sekta hii ya kilimo kwa kuwapa mashamba kulima kwenye hizo block farming na kuwezesha miundombinu yote ili tuzuie fujo zilizo mitaani? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Intergrated Labour Force Survey inasema nchi yetu ina takribani ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi milioni 22.3 ambao asilimia kubwa ni vijana. Sisi kama Wizara ya Kilimo tumeona kundi hili kubwa tukilitumia vizuri lina uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu na kuikuza sekta ya kilimo. Kufuatia hayo Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa bajeti yake kuanzia mwezi Julai tunakuja na utekelezaji wa program maalum ambayo itawahusisha vijana nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, program hii itakuwa ni kuwapatia vijana maeneo kwa maana ya mashamba makubwa ya kilimo kuwasaidia kupata mitaji, kuwasaidia pembejeo na kuwatafutia pia masoko na kwa kuanzia tumepata eneo la hekari 20,000 katika Wilaya za Chamwino na Bahi na mradi huu utaanza mwezi Julai, kama sehemu ya majaribio na baadaye utakwenda nchi nzima ili kuwafikia vijana wengi zaidi. (Makofi)

Name

Venant Daud Protas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igalula

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 3

MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi. Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ilitekeleza agizo la Serikali la kuengeneza block farming, ikaandaa hekari 15,000 katika kijiji cha Kalangazi na aliyekuwa Naibu Waziri na sasa ni Waziri wa Kilimo alituahidi ataleta Shilingi Bilioni tano na trekta. Je, ni lini Serikali itatekeleza block farming ya Kalangazi ili ianze kuleta tija kwa uchumi wa nchi? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Venant Protas, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yetu wakati tumeisoma hapa Bungeni tulisema, moja kati ya malengo yetu makubwa ni kufikisha mashamba makubwa 10,000 ifikapo mwaka 2030. Kwa hiyo, popote panapotokea fursa ya uanzishwaji wa mashamba makubwa sisi tupo tayari kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya namna hiyo. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge jambo hili alishalisema baada ya Bunge la Bajeti, mimi na yeye tutaongozana kwenda Uyui kuangalia eneo hilo na baadaye tutashirikiana na wataalam kwa ajili ya utekelezaji.

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa?

Supplementary Question 4

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza niwashukuru Wizara ya Kilimo kwa kazi nzuri wanazofanya. Wakulima wa pamba maeneo wanakolima pamba hasa katika Jimbo la Ushetu wamekuwa na changamoto kubwa sana ya maghala ya kuhifadhia pamba na madhara yake pamba hii inachafuka sana na kuhatarisha soko letu la ndani na la nje. Je, ni lini sasa Serikali itawajengea maghala ya kudumu wakulima wa pamba hapa nchini, hasa katika Jimbo la Ushetu ili waweze kuhifadhi pamba yao ili kulinda soko letu la ndani? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja kati ya mikakati tuliyonayo ni kuhakikisha tunapunguza post harvest loss kutoka asilimia 35 ilivyo hivi sasa kurudi tarakimu moja. Mkakati uliopo ni ujenzi wa maghala ya kutosha, ndio maana kwenye bajeti yetu tuliyoisoma hapa Bungeni, bajeti ya ujenzi wa maghala imetoka Shilingi Bilioni mbili mpaka Shilingi Bilioni 25 lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na ujenzi wa maghala mengi zaidi. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba tunaangalia maeneo hayo yote hasa ya uzalishaji ili tuweze kuwa na maghala ya kutosha na tuweze kuhifadhi mazao yetu ya kilimo katika mfumo mzuri.