Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- Je, kwa nini Kodi ya Jengo na Kodi ya Ardhi zisiunganishwe na kuwa moja ili kumwondolea usumbufu mwananchi?
Supplementary Question 1
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kuishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri, lakini naomba niulize maswali mawili ya ziada.
Swali la kwanza, kwa kuwa suala la utafiti ni suala linalochukua muda, je, Serikali inaweza ikawaambia wananchi ni lini wanategemea kumaliza utafiti huu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu mifumo ni jambo kubwa, je, Serikali iko tayari kuendelea kutoa taaluma zaidi kwa wadau ambao wanasumbuka sana na mifumo hii? Ahsante sana.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zahor, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, tathimini hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu ndani ya mwaka huu na Bunge hili la Bajeti.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Serikali kupitia taasisi zake imekuwa na utamaduni na imekuwa na desturi ya kutoa mafunzo siku hadi siku kwa wadau wanaostahiki, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved