Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Norah Waziri Mzeru
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wadau wa michezo kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu?
Supplementary Question 1
MHE. NORAH W. MZERU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kujenga na kuboresha viwanja vya michezo nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu je, Serikali imejipangaje kuendeleza vipaji vya vijana hao? (Makofi)
Swali la pili, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga na kuboresha viwanja vya michezo mashuleni na kwenye vyuo? Ahsante. (Makofi)
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru Mheshimiwa Norah kwa maswali yake mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, mpango wa Serikali kuendeleza vipaji, kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, Serikali kwa kushirikiana na TFF tunaandaa mashindano mbalimbali ya vijana ili vipaji ambavyo vimeweza kupatikana viweze kukuzwa na kuendelezwa kupitia mashindano hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kuna ligi ya under 17, lengo ni kuonesha vipaji hivyo vinakuwa vipi, tuna UMISETA na UMITASHUMTA ambayo kesho Mheshimiwa Waziri Mkuu ataenda kufungua kule Tabora. Mashindano hayo yote yana lengo la kuhakikisha kwamba vipaji vinavyopatikana vinaweza kuendelezwa. Katika kituo cha TFF Tanga na Dar es salaam mafunzo ya kuendeleza vipaji hivyo yanaendelea na hata hivi sasa ninavyoongea wataalamu wapo wanatoa mafunzo hayo. Kwa hiyo, tunahakikisha vipaji hivyo vitaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali la pili, katika bajeti tuliyopitisha mwaka huu tarehe 23 Mei, tulisema Serikali ina mpango wa kujenga shule 56 ili kuzibadilisha kuwa shule za michezo. Shule hizo 56 ambazo zitakuwa ni shule mbili katika kila mkoa Tanzania Bara na Visiwani zitakuwa ni mahususi kwa kuchukua vipaji hivyo na kuviendeleza, lakini kuendeleza miundombinu ya michezo katika mashule hayo. (Makofi)
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wadau wa michezo kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, moja kati ya wadau wakubwa wa michezo ni Serikali na Serikali ina shule zake za sekondari na za msingi wanafunzi wengi hawana vifaa vya michezo.
Je, Wizara haioni sababu ya kuwa na mkakati wa makusudi wa kuwasiliana na Wizara ya Fedha mkashusha kodi kwenye vifaa vya michezo shuleni ili ku-support watoto wapate vifaa vya michezo kwa sababu imekuwa ni changamoto kubwa kwenye Taifa letu? (Makofi)
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na namshukuru Mheshimiwa Festo Sanga kwa ufuatiliaji mzuri wa maendeleo ya michezo.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni Serikali kwa kushirikiana na TFF tumegawa mipira 1,000 kwa ajili ya wanafunzi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani. Tumepokea wazo lake, tutaongea na Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba tunatoa au kupunguza kodi katika vifaa vya michezo ili vijana hao wengi na Watanzania kwa ujumla waweze kumudu vifaa hivyo. (Makofi)
Name
Tarimba Gulam Abbas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kinondoni
Primary Question
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wadau wa michezo kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu?
Supplementary Question 3
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nimefurahi kusikia kwamba Tanzania tuna ligi ya under 17 lakini ligi hii haionekani kuwa promoted.
Je, Serikali haioni haja sasa ya kuvitaka vilabu vya premier league kulazimishwa kuwa na timu za under 17 ambazo zinashiriki katika hiyo premier league?
Name
Halima James Mdee
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas kwa mchango wake kuendeleza michezo. Nilimwona akishangilia kombe lile la Yanga hivi juzi, lakini ningemwomba pia angeshangilia na lile la Simba la Muungano. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali lake la msingi, ligi ya under 17 inaendeshwa na vilabu vya championship, league under 20 inaendeshwa na vilabu vya premier league lakini nimepokea wazo lake kwamba vilabu vya premier league sasa navyo viwe na league ya under 17 na league ya under 14 katika mkakati wa kukuza na kuibua vipaji. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved