Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 1

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ningependa kujua pamoja na kupata hii miradi, lakini utekelezaji wake hadi sasa bado haujafanyika. Kwa hiyo, ni lini sasa Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kunihakikishia utekelezaji utaanza?

Mheshimiwa Spika, la pili kuna baadhi ya maeneo mengine ambayo pia yana changamoto ya mawasiliano ikiwemo Kata ya Maghojoa, Kinyagigi, Kinyeto na katika Vijiji vya Minyaa na Kimbii. Ni lini sasa Mheshimiwa Waziri anaweza akanipatia miradi ya minara katika maeneo haya ili wananchi wetu waache kutaabika? Ahsante.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ameuliza ni lini utekelezaji utaanza? Tunatarajia mwaka ujao wa fedha maeneo haya yote uliyoyataja Mheshimiwa Mbunge tunakuja kuyafanyia tathmini na kuweza kuyapatia huduma, lakini katika Kata hizi za Kinyeto na kata nyingine ulizozitaja UCSAF inakuja kufanya tathmini na lengo ni kuhakiki uhitaji halisi, ni lazima huduma iweze kufikia maeneo haya yote. Kadiri tutakavyopata fedha kuanzia mwaka ujao wa fedha tutahakikisha wananchi nao wanapata huduma nzuri ya mawasiliano. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 2

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Naibu Waziri alienda Nyamuhonda, Mwema na Itiryo hakuna mawasiliano kabisa na watu wanasikiliza redio na Tv ya Kenya. Ni lini minara itawekwa katika maeneo hayo ili tupate mawasiliano ya Tanzania? Ahsante. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, UCSAF inaendelea kufanya tathmini maeneo mbalimbali hasa haya ya mipakani. Mheshimiwa Waitara naomba nikuahidi maeneo haya yote uliyotaja nayo tutayafikia ili waweze kupata huduma ya minara kutoka Tanzania.

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 3

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Wilaya Mbogwe ina kata 17, Makao Makuu ya Kata ya Mbogwe hakuna mawasiliano na Kata za Nanda, Nhomolwa pamoja na Lulembela na maeneo mengine ya kiuchimbaji.

Mheshimiwa Spika, naomba kumwuliza Naibu Waziri, ni lini utekelezaji wa minara hii utaenda kujengwa na Serikali?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Nicodemas kutoka Mbogwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, makao makuu ya wilaya na maeneo yanaizunguka yanakosa mawasiliano ya uhakika. Mheshimiwa Mbunge tuko katika mchakato wa kuhakikisha minara inafika maeneo yote muhimu yenye population kubwa na pia sehemu za pembezoni. Kwa hiyo, maeneo haya ya Mbogwe pia ni moja ya maeneo ambayo tutawaletea mawasiliano.

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 4

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, naomba niulize Serikali maeneo ya kwangu maeneo ya Muhanga, Gurungu, Turieli na Mnazi Mmoja pamoja na Kitanula hakuna kabisa mawasiliano, je, Serikali ipo tayari kupeleka minara katika maeneo haya ili wananchi nao waweze kufaidi matunda ya nchi yao? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Yahaya kuwa tupo tayari kuleta mawasiliano maeneo haya na tayari michakato ya kuja kufanya tathmini tupo mwishoni kuja kufika maeneo haya yote.

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 5

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Spika, naomba kujua ni lini Kijiji cha Chagu, Kalilani, Songambele na Ikuburu watapata mawasiliano? Ahsante.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunikumbusha.

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza katika Kijiji cha Songambele na vijiji vyote ulivyovitaja Mheshimiwa Nashon tunakuja kuleta minara na kuhakikisha mawasiliano yanakuwa murua.

Name

Khalifa Mohammed Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Mtambwe

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 6

MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, baadhi ya vijiji vya Jimbo la Mtambwe havina mawasiliano ya simu kabisa. Je, ni lini mtaleta wataalamu wenu kuja kuvitambua na kuvipatia mawasiliano ya simu?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza kuwa maeneo ya Mtambwe mwaka ujao wa fedha mapema kabisa wataalamu watakuja kufanya tathmini ili kujua uhitaji ambao unatakiwa katika eneo hili na kuleta mawasiliano.

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 7

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mji wa Mwanza umeendelea kukua kwa kasi na watu wameongezeka na kujenga maeneo ya pembezoni, Serikali ipo tayari sasa kufanya upya tathmini ya mawasiliano na kupeleka minara?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante, tupo tayari kufanya tathmini mpya.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 8

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali iliweka minara katika maeneo ya visiwa base ambako kulikuwa hakuna mawasiliano, sasa hivi mawasiliano wanapata, changamoto waliyonayo hawana zile voucher za kukwangua na si wote waliozoea kununua kwa kutumia simu. Ni lini voucher hizo zitapatikana ili mawasiliano yao yawe mazuri? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza kuhusu vocha za kukwangua, naomba niseme nimelipokea nitalifikisha kwa watoa huduma lakini kama Serikali tunaendelea kutaka kuboresha kuondokana na hizi hard copies na kuingia kwenye voucher moja kwa moja kupitia mtandao.

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?

Supplementary Question 9

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Kiwombi - Kata ya Amanimakoro, Kijiji cha Sala - Kata ya Muhongozi, Kijiji cha Kihangimauka - Kata ya Kihangimauka, vijiji hivi vilikuwa na makubaliano na UCSAF lakini hadi leo hakuna kinachoendelea. Ni lini minara hii inaenda kujengwa?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nikupongeze Mheshimiwa Mbunge hili suala tumeliongea jana tu na tumeshakubaliana mimi na wewe tutakwenda, lakini nimeshatoa maagizo kwa Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini anashughulikia hii minara. (Makofi)