Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Mahakama mpya katika Kata za Chala na Kate Jimbo la Nkasi?

Supplementary Question 1

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nina swali moja la nyongeza. Kata ya Kipande na Kata ya Sintali wananchi wanatembea umbali mrefu na wanatumia muda mrefu kufuata huduma za Mahakama. Lini mtajenga Mahakama katika Kata ya Sintali na Kipande? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali la Mheshimiwa Mbogo, Mbunge wa Nkasi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wapo wananchi wanatembea umbali mrefu hasa kwenye maeneo yenye mtawanyiko wa watu kama Jimbo la Mheshimiwa Mbunge. Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, kadri tutakavyopata fedha tutaendelea kupeleka huduma hizi za Mahakama kwenye maeneo ambayo hayana kabisa ikiwemo kata hizi alizozitaja za Kipande na Sintali. Ahsante.