Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Jumanne Mtemvu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibamba
Primary Question
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza: - Je, hadi sasa Serikali ina madeni kiasi gani ya watumishi wa umma yanayohusu likizo, uhamisho na kusafirisha mizigo baada ya kustaafu?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ningeomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Serikali inasimamiwa na Mwongozo wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 zinazotaka madeni ya watumishi wa umma yanapotokea tu yalipwe ndani ya miezi 12. Je, ni lini Serikali itasimamia mwongozo huu wa kikanuni?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa madai mengine ya wazabuni na wakandarasi yanapochelewa kulipwa hulipwa na riba. Je, Serikali haioni haja sasa ije na sera na sheria hapa Bungeni ili iweze kuweka hiyo nafasi ya kuchelewa kulipa itawalipa na riba watumishi wa umma ili hiyo haja ya kuwalipa iende kwa kasi? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo unaozungumzwa na Mheshimiwa Mbunge wa mwaka 2009 ni mwongozo unaohusu udhibiti wa ongezeko la madeni ya Serikali kwa watumishi wa umma. Ni kweli maneno kama anayosema Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilieleza kwamba pamoja na mazingatio mengi ambayo yameelezwa ndani ya mwongozo huu, lakini moja ya jambo la msingi kabisa ni kuhakikisha kwamba Serikali inakuwa na mpango mzuri kwa ajili ya kurithisha madaraka na mara nyingi huo mwongozo unafanywa kwa kupitia bajeti zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika swali lake la kwanza kwamba Serikali inaendelea kusimamia mwongozo huu na pale ambapo panatokea mapungufu Serikali kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu - Utumishi imekuwa inapeleka maelekezo na kuendelea kukumbusha juu ya wale maafisa uajiri kuendelea kusimamia mwongozo huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, madeni haya yanalipwa lini? Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imejipanga vizuri. Nataka nikutoe wasiwasi wewe, lakini pia kulitoa wasiwasi Bunge lako kwamba Serikali inaendelea kusimamia mwongozo huu na kuhakikisha kwamba madeni yote yale ambayo yamehakikiwa na taarifa zake zimeletwa katika mamlaka husika kwa ajili ya malipo, tunafanya hivyo.
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza: - Je, hadi sasa Serikali ina madeni kiasi gani ya watumishi wa umma yanayohusu likizo, uhamisho na kusafirisha mizigo baada ya kustaafu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika Mkoa wetu wa Iringa ulifanya ziara na hii changamoto ilijitokeza karibu katika wilaya zote za Mkoa wetu wa Iringa na wafanyakazi kwa kweli wanapata shida sana kwa sababu wanashindwa hata kutafuta nyumba nyingine kwa ajili ya kuhamia na wengine wameshindwa kusafirisha mizigo yao kule ambapo inatakiwa waende ambapo wameshastaafu.
Je, ni kwa kipindi gani anatakiwa adai haya madai yake kwa sababu yanakuwa yanachukua muda mrefu kiasi kwamba wanapata mateso makubwa sana? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kipindi gani mfanyakazi anatakiwa kudai madeni haya? Jambo la msingi narudia tena kwamba mwongozo wa mwaka 2009 umeelekeza waajiri wote kwamba kabla hamjapandisha watu madaraja, kabla mtu hajastaafu ni vyema mwongozo huu ukafuatwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo upo wazi kabisa ambao unaelekeza nini kifanyike kabla hatujafika kwenye kudai madeni. Kipindi gani madeni haya yanatakiwa kulipwa? Nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba madeni haya yanatakiwa yadaiwe muda wowote ambao mtu anastahiki kulipwa stahiki zake kwa mujibu wa mwongozo ambao umetolewa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved