Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, lini kongani za korosho za Maranje Nanyamba zitajengwa ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais alipotembelea Mkoa wa Mtwara?
Supplementary Question 1
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwanza naomba kuishukuru sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kulipa fidia wananchi wa Nanyamba, Maranje na pia kwa kupeleka fedha shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi. Nina swali dogo tu moja la nyongeza.
Kwa kuwa sasa mradi huo umeanza kutekelezwa na wanawake wa Mkoa wa Mtwara wakiwemo wanawake wa Tandahimba, Newala na Mtwara Vijijini yenyewe ndio wanaobangua korosho kwa sasa kwa kutumia mashine ndogo ndogo.
Je, Serikali imeweka mpango gani wa kuhakikisha hao wanawake wabanguaji wanaotambulika tayari waingie kwenye huo mfumo mara hiyo kongani inapoanza?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Agnes Hokororo kwa kuwatetea wanawake katika mkoa wake na hususani maeneo ya Tandahimba, Mtwara na Newala. Nimthibitishie tu kwamba wanawake wote wanaotokea maeneo yanayozalisha korosho ndio watakaokuwa sehemu ya wanufaika wa mradi huu. Katika mradi ule kuna maeneo ambayo tutatenga ili na wao waweze kuwa sehemu ya mradi huo kwa sababu tunahitaji na wao kuongezewa thamani ya korosho pamoja na kupata kipato, ahsante.(Makofi)
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, lini kongani za korosho za Maranje Nanyamba zitajengwa ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais alipotembelea Mkoa wa Mtwara?
Supplementary Question 2
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Mimi niipongeze Serikali kwa kulipa fidia kwa wakati na kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Swali langu ni kwamba kwa kuwa mradi ule andiko la awali linasema kutakuwa na ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 20,000, je, Serikali imejipangaje katika kupeleka huduma nyingine, hususani huduma za afya, ujenzi wa kituo cha afya pale Maranje, ni lini Serikali itafanya kazi hiyo?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, najua eneo la Mheshimiwa Mbunge ndilo ambalo tunalifanyia kazi na ameuliza hivi ikiwa ni sehemu ya kuwatetea wananchi katika eneo lake. Nimhakikishie tu katika ule mradi kwenye ile design ndani ya ule mradi kuna kituo cha afya. Kwa hiyo, lipo na tutalitekeleza, ahsante.
Name
Tunza Issa Malapo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, lini kongani za korosho za Maranje Nanyamba zitajengwa ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais alipotembelea Mkoa wa Mtwara?
Supplementary Question 3
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, katika kuelekea utekelezaji wa mradi huo mkubwa na mzuri, nataka kujua Serikali imejifunza nini? Kwa sababu Mtwara kulikuwa na viwanda vya korosho, vingi vimekufa na vimefungwa yaani wakati mnakwenda kutekeleza huo mradi mmejifunza nini ili mradi huo uweze kufanya kazi vizuri?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kitu kikubwa ambacho Serikali tumejifunza ni kwamba moja ni kuongeza usimamizi thabiti katika yote ambayo Serikali tunayaanzisha. Sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha huo mradi unakamilika, tutausimamia na utakuwa endelevu. Haitakuwa ile miradi ambayo tukishaianzisha na baadaye tunaiacha na inakufa. Kwa hiyo, tuamini sisi kwa sababu hili jambo liko ndani ya uwezo wetu, tumekwishalifanyia studies za kutosha na litakamilika kwa wakati kama ambavyo tumejipanga.
Name
Katani Ahmadi Katani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tandahimba
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, lini kongani za korosho za Maranje Nanyamba zitajengwa ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais alipotembelea Mkoa wa Mtwara?
Supplementary Question 4
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, vile viwanda ambavyo viliuzwa na Serikali kwa dhamira ya kuendeleza ubanguaji na walionunua viwanda hawakufanya ubanguaji na badala yake wamefanya maghala.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuvirejesha viwanda vile kwa sababu havijafanyiwa kazi iliyokusudiwa?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhusiana na uongezaji thamani kwenye sekta hii ya korosho. Kimsingi ni kweli viwanda vingi ambavyo vilikuwa vimebinafsishwa wakati ule ambavyo viko kwenye sekta ya korosho, walionunua wengi/waliobinafsishiwa hawakuviendeleza na moja ya anachokisema Mheshimiwa Katani ni kweli na tumeshasema tayari Serikali imeshaanza mchakato wa kuvirejesha viwanda vyote ambavyo viliuzwa au vilibinafsishwa na havifanyi kazi na walionunua hawajaviendeleza. Kwa hiyo, naomba tu watupatie nafasi tukamilishe mchakato huu ili tuvirejeshe Serikalini na kuwatafutia wawekezaji wengine.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved