Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Serikali iliahidi kuunganisha Mkoa wa Kagera na Gridi ya Taifa, lakini mpaka sasa ni zaidi ya miaka miwili mitatu hivi. Ni nini mkakati wa Serikali au wamefikia hatua gani kuunganisha Mkoa wa Kagera na Gridi ya Taifa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; maeneo mengi yaliyopitiwa na REA Awamu ya Pili ambapo kwa Kyerwa ilikuwa ni Awamu ya Kwanza walipitisha laini kuu. Kwa hiyo, maeneo mengi hayajapewa umeme. Je, ni lini Serikali itawapelekea wananchi ambao walikatiwa migomba yao na mibuni ili na wao waweze kupata umeme?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sebba Bilakwate kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze na swali la pili ambalo lina mahusiano makubwa sana na swali la msingi. Kule kwenye awamu ya pili ya upelekaji wa umeme kuna vijiji ambavyo viliachwa. Katika awamu hii ya tatu, mzunguko wa pili vijiji vyote vilivyokuwa vimeachwa sasa vimechukuliwa. Kwa hiyo, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Bilakwate kwamba vijiji vyake vyote ambavyo nakumbuka vipo 29 viko katika Mradi wa REA, awamu ya tatu, mzunguko wa pili na umeme utafika katika vijiji vyote hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye eneo la vitongoji ambavyo sasa viliachwa na awamu ya pili na vimeachwa na awamu ya tatu ni kama tulivyoeleza, azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba sasa vitongoji vyote vinazidi kupelekewa umeme kwa kulingana na upatikanaji wa fedha na ule mkakati mkubwa ambao tayari tulishaueleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la gridi ya Taifa, azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kwamba kufikia mwaka 2025 mikoa yote na maeneo yote ambayo hayakuwa na gridi ya Taifa yawe yamefikiwa na gridi ya Taifa. Kwenye bajeti yetu tulieleza vizuri kuhusu Kigoma na Katavi. Kwenye Mkoa wa Kagera gridi ya Taifa inatarajiwa kutolewa eneo la Benako kuletwa mpaka Kyaka kwenye ule Mradi unaotokea kule Rusumo. Tayari fidia imeshafanyika kwenye maeneo hayo na taratibu nyingine za kiujenzi zinaendelea na mradi utafanyika kwa ajili ya faida ya Wanakagera.

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 2

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, lini Serikali itapeleka umeme katika Vitongoji vya Nyamwilonge, Lutenga, Kavungwe katika Kata ya Nyantukuza, Bwela Kata ya Muhange, Nyakavilu Kata ya Gwarama katika Wilaya ya Kakonko? Ahsante.

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aloyce Kamamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, vitongoji ambavyo havina umeme vipo katika awamu mbalimbali za kupelekewa umeme kulingana na upatikaji wa fedha, lakini tunao Mradi wa REA III Round II ambao unaendelea kupeleka umeme katika vijiji vyetu inawezekana kabisa kuna baadhi ya vitongoji ambavyo vitaguswa na mradi huo. Kwa vile ambavyo havitapata, kama tulivyosema tunatafuta fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kupeleka umeme kwenye vitongoji vyote kwa wakati mmoja tulivyosema kwenye bajeti iliyopita Sh.6,500,000,000,000 kwa ajili ya kufanikisha mradi huu wote. Serikali ya Awamu ya Sita inayo azma ya kufanya kazi hii na tunaamini tutafanikiwa.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 3

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Kasi ya Mkandarasi wa Wilaya ya Tanganyika aliyepewa dhamana ya kupeleka umeme vijijini hasa kwenye maeneo ya Vijiji vya Mishamo ambako Mheshimiwa Naibu Waziri alifika na kuzindua kasi yake ni ndogo sana.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili Mkandarasi aweze kukamilisha huo mradi na wamsimamie ili amalize kazi yake kwa wakati?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakoso, Mbunge wa Tanganyika, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nitoe wasiwasi au niweke taarifa sahihi kwamba fedha za utekelezaji wa Mradi wa REA III Round II Sh.1,240,000,000,000 ipo na hakuna uhaba wa fedha katika eneo hili. Pia, kwa yale maeneo ambapo tumeona kuna mabadiliko na ongezeko la bei tayari Serikali imeshatoa fedha, tunakamilisha taratibu za majadiliano ili tuweze kuongeza fedha hizo kwa ajili ya Wakandarasi kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu tunaoutumia sasa ni wa Mkandarasi anafanya kazi, tunakagua, tunamlipa na tayari Wakandarasi wote walishapewa advance payment ambazo hawajazifanyia kazi na kuisha. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba ufuatiliaji unafanyika na kwenye bajeti tulieleza mbinu mpya ambazo tumeziweka kwa ajili ya usimamizi wa karibu. Nimhakikishie kwamba kazi itaendelea baada ya hizi taratibu za marekebisho ya bei ya mikataba kukamilika, maeneo yote yataonekana kufanyiwa kazi kwa spidi zaidi na tutasimamia kuhakikisha tunamaliza kazi kwa wakati.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Mitaa ya Msisina, Mtalagala, Kivululu iliyopo katika Manispaa ya Iringa haijawahi kupatiwa umeme toka ilipohamishiwa kutoka Jimbo la Isimani. Je, ni lini sasa Serikali itaona umuhimu wa kuwapatia umeme kwa sababu ilikuwa ipatiwe umeme wa REA lakini mpaka leo haijapatiwa?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye maeneo ya mijini tunao mradi ambao unakamilika manunuzi yake na tunatarajia utaanza mwezi Julai, 2022, unaoitwa peri-urban. Kwa hiyo, kama anavyosema ni mitaa ambayo ilitoka katika jimbo lingine na kuja mjini, tunaamini ipo katika mradi huo na itapelekewa umeme kupitia huo Mradi wa Peri-urban ambao unasimamiwa na REA.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelekezo ya Serikali ni kuhakikisha kwamba TANESCO inaendelea kupeleka umeme katika mitaa yote na vijiji vyote ambavyo pengine miradi mingine haijafika. Kwa hiyo, maeneo hayo tutaendelea kuyapelekea umeme na nitaomba tuwasiliane baada ya hapa ili tuweze kujua specifically eneo hilo liko kwenye mradi gani na ufuatiliaji uweze kufanyika ili umeme uweze kufika.

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 5

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Ndani ya Jimbo la Kibamba wapo wananchi wengi sana ambao walilipia Sh.27,000 waunganishiwe umeme, lakini mpaka sasa wamekuwa wakisumbuliwa na bado hawajaunganishiwa. Je, Serikali ipo tayari kutoa maelekezo katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Kimara na Kibamba ili wananchi hao waunganishiwe umeme haraka?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Issa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunakiri kwamba kuna watu ambao walishalipia huduma ya umeme lakini walikuwa hawajaunganishiwa. Nitoe maelezo katika maeneo mawili, agizo la kwanza kwa wenzetu wa TANESCO ambao tayari walishalipata; ni kwamba hakutakuwa kuna mabadiliko ya bei, yule ambaye alishalipia gharama ataunganishiwa kwa gharama hiyo hiyo. Nasisitiza kwamba yeyote atakayeambiwa ulilipa Sh.27,000 lakini sasa unatakiwa ulipe zaidi tupatiane taarifa ili tuweze kufanya ufuatiliaji na kuwajibishana katika eneo hilo. Yeyote aliyelipa shilingi 27,000 ataunganishiwa kwa gharama hiyo hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande huo huo, ni kweli kwamba tunayo load kubwa ya wateja ambao wamelipia na tunaendelea kuhangaika nayo na tuna mkakati wetu wa kuhakikisha kwamba hatuwi na backlog ya zaidi ya mwezi mmoja; kwa sababu Serikali ya Awamu ya Sita sasa imetuwezesha kupata fedha za kutosha kwenda kupeleka umeme, namhakikishia Mheshimiwa Mtemvu kwamba tutafanya kazi hiyo na uunganishaji utakamilika kwa wakati.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Supplementary Question 6

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niuulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati walipokuja wataalam wa TANESCO hapa Bungeni tuliwapa list ya maeneo ambayo kwetu Namtumbo yalirukwa kwa ajili ya kuweza kuingizwa ili yaweze kuwekewa umeme. Kwa mfano; Ligunga, Lusewa, Likuyu Seka katika maeneo ya Selous, Likuyu Water Pump pia Ulamboni Ligela, Muungano na Mgombasi. Mpaka leo asubuhi hii bado yule Mkandarasi anasema hajapatiwa approval kutoka REA nasi tulipeleka TANESCO.

Je, Serikali inaweza ikawasukuma TANESCO waipeleke REA na ipate approve ili hivi vijiji na maeneo yaliyorukwa ya taasisi yaweze kuingizwa Mkandarasi afanyekazi yake sasa hivi? (Makofi)

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Vita Kawawa na niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge wote kwamba, katika Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili ya upelekaji wa umeme vijijini hakuna kijiji hata kimoja kitakachobaki bila kupelekewa umeme. Kwa hiyo, yale maeneo machache ambayo yalikuwa yamebakia yanafanyiwa analysis na upembuzi na taratibu zikishakamilika yataingizwa pia katika maeneo yetu ya kutengeneza mikataba kama additional scope of work. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kawawa kwamba jambo hili linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, haikuwa tu rahisi kumwambia Mkandarasi peleka hap, hatujajua urefu ni kiasi gani, upana ni kiasi gani ni lazima pia tujiridhishe lakini kazi hiyo itafanywa na Mkandarasi aliyeko site na kabla hajamaliza kazi yake atakuwa amefanya pia katika maeneo hayo. (Makofi)