Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwanza; kwa kuwa matibabu ya kusafisha figo ni gharama kubwa ni kuanzia shilingi 145,000 mpaka 350,000 na gharama hiyo ni kubwa sana kwa Mtanzania wa kawaida, kwa kuwa Serikali mnaelekeza kwamba, mpaka Muswada utakapokuja wa Bima ya Afya kwa wote ndiyo tuangalie punguzo la hilo.

Je, Serikali kwa nini sasa kwa wale ambao wameingia mpango wa Bima ya Afya kujipimia tena wana vifurushi vikubwa, wasipewe huduma hiyo mpaka tusubiri huo Muswada wa Bima ya Afya kwa wote jambo ambalo ni gumu kama mmeshindwa kwa wachache mtaweza kwa wengi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa matatizo haya ya figo yanakua kwa kasi, na tafiti zinaonesha kwamba zilizofanyika katika Mikoa ya Kaskazini asilimia 6.8 ya Watanzania wana magonjwa ya figo pasipo kujitambua.

Je, Serikali imejipanga vipi sasa katika kutoa elimu kwa wananchi wake kujua dalili na matatizo hayo yanatokana na nini, kwa sababu yanakuja ghafla? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge.

Kwanza, kwamba kuna watu wanaolipa kifurushi kikubwa cha Bima ya Afya na kwa nini wanashindwa kupata hiyo huduma. Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshaelekeza kwamba watu wanaokata vifurushi vyao wapate hiyo huduma. Kwa sababu tujiulize maswali, ukienda kwenye private sector utakuta bei ni ileile na ukirudi kwenye Serikali bei ni ileile, lakini wakati huo private sector wao wenyewe ndiyo wananunua vifaa, wanajenga na wanafanya mambo mengine na kulipa mishahara. Serikalini, kujenga na kununua vifaa vinafanyika na Serikali, kwa maana hiyo ndiyo maana Waziri wa Afya ameita timu ya kukaa chini ili kujadili ni namna gani tuweze siyo tu kuwasaidia wale wenye vifurushi vikubwa vya bima lakini hata wagonjwa wengine wasio na bima, ishuke kabisa hata ikiwezekana kuwa Shilingi 50,000 kwa mtu mmoja badala ya bei ya Shilingi 900,000 kwa wiki ambayo ipo sasa. Kwa hiyo, Waziri analifanyia hilo kazi na siyo muda mrefu tutapata majibu kuanzia tarehe Mosi Julai, 2022. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli hata kwa dunia, sisi kwetu ni asilimia Sita ya watu wanaonesha kuna hilo tatizo lakini kwa dunia ni asilimia 10, ni tatizo la kidunia siyo la Tanzania peke yake. Kwa hiyo, kimsingi Serikali inajipanga moja kuhakikisha kwamba tunatoa elimu kama unavyosema na wewe ni mmojawapo wa mdau ambaye wa kutusaidia kwa sababu kuna masuala mazuri kwamba sisi wenyewe tujipange namna tunavyokula, kufanya mazoezi na mambo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Serikali ndiyo maana unaona kuna mjadala mkubwa wa usalama wa chakula na usalama wa madawa. Tunakwenda kuboresha eneo la usalama wa chakula ili kuhakikisha kwamba tunapunguza matukio kama haya, lakini utaona hamasa kubwa iliyokuwa inafanyika hasa wakati wa Corona tufanye mazoezi, tule vizuri, tuhakikishe kwamba tunakula vyakula ambavyo siyo vya protini za wanyama tule zaidi protini za mimea na vitu vingine kama hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukifanya hivyo nasi Wabunge tunapofanya mikutano yetu tuendelee kuhamasisha zile tabia nzuri za afya, mimi naamini tutapunguza haya matatizo ambayo yanatokea. Pia wote tuwe wadau hasa kwenye suala zima la usalama wa chakula na masuala ya chakula kuingia na kufikiriwa katika angle ya kibiashara zaidi badala ya kufikiriwa kwenye angel ya usalama wa nchi hatutaweza kutoka, ndiyo maana nasema tushirikiane pamoja kuhakikisha wafanyabiashara hawatusukumi hasa kwenye eneo la chakula, vyakula vyote vinavyozalishwa na wadau ni kusimamia usalama, tuungeni mkono.

Name

Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 2

MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Naibu Spika, tunazo taarifa kwamba Mheshimiwa Rais amenunua mashine za kusafisha figo 171. Je, hospitali hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere maarufu kwa jina la Kwangwa itapata mgao huo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Rais wetu Samia Suluhu Hassan amenunua mashine 171 na mashine 110 zimeshasambazwa kwenye hospitali 11 na sasa Waziri wetu Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameshaelekeza mashine 11 ziende kwenye hospitali aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 3

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Kwa kuwa, maradhi ya figo ni tishio hata kwa vijana wetu; je, Wizara imejipanga vipi kutoa elimu mashuleni ili kukinga wanafunzi wetu na vijana wetu wasiambukizwe na maradhi haya? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake zuri alilouliza Mheshimiwa Mbunge, Moja, Mheshimiwa Waziri wa Afya ameshaelekeza kwamba pamoja na elimu tushirikiane na Wizara ya Elimu, Wizara ya Kilimo kwenye kutoa elimu moja kwa moja mashuleni, pia Wizara ya Kilimo tunashirikiana nayo kwa maana ya masuala mazima ya lishe bora na uzalishaji kule chini, tukishirikiana Wizara mbalimbali naamini na kwenye mitaala yetu tutaboresha eneo hilo la afya na watu watajua. Pia Idara ya Elimu ya Afya kwa Umma iwe na utaratibu wa kufikisha elimu kwa wahusika. (Makofi)

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 4

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Askari wetu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Bima zao zinawaruhusu kutibiwa katika hospitali za Jeshi peke yake, na hospitali hizi za Jeshi haziko kila mahala nchini. Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa ku-extend bima zao ili waweze kutibiwa kwenye hospitali zingine pia? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake ni la msingi sana na kwa sababu linahusu Wizara mbili, Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Afya tunalichukua na tunaitana mara moja kulijadili hilo ili kuweza kurahisishia Jeshi letu kupata huduma kwa urahisi. (Makofi)

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 5

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 40 ya vifo hapa nchini inatokana na magonjwa yasiyoambukiza, haya magonjwa yasiyoambukiza yana gharama kubwa pia kwenye matibabu yakiwemo moyo, kansa, figo na kadhalika. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba haya magonjwa yasiyoambukiza wananchi wanapewa elimu ya namna ya kuishi ili kuepukana na hiyo gharama kubwa ya matibatu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali ni mkakati wetu wa siku zote wa Elimu ya Afya kwa Umma. Ni kweli kwamba ni gharama kubwa sana matibatu ya moyo na vitu vingine. Kwa mfano, ukizungumzia moyo ni kwa sababu ya teknolojia inayotumika, Serikali inaingia gharama kubwa sana kwenye kununua teknolojia yenyewe kama teknolojia inayosaidia kwa mfano umeme wa moyo unakuta ni teknolojia ya hali ya juu, kwa hiyo, suluhisho letu ni bima ya afya kwa wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nimuombe Mheshimiwa Mbunge yeye ni mdau na Bunge zima tuendelee pamoja kuhamasisha masuala ya afya na masuala ya magonjwa yasiyoambukiza kwa sababu Wizara ya Afya wakati wote imekuwa ikilijengea Bunge uwezo na lengo letu ni kufikisha huduma kule chini.

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wagonjwa wa figo kupata matibabu ya kusafishwa figo kwa gharama nafuu?

Supplementary Question 6

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona.

Kwa kuwa, wagonjwa wa figo wa Mkoa wa Kagera wamekuwa wakipata shida sana kufuata huduma hii ya kusafisha figo hospitali ya Bugando. Je, ni lini Serikali italeta mashine katika Mkoa wetu wa Kagera? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika hospitali 11 ambazo zimepata mgao na hospitali ya Kagera ni mojawapo. Ni kwamba kinachongojewa ni kumaliza ujenzi wa jengo la kufanya hiyo huduma, jengo likimalizika vifaa vyake vipo ni kufunga tu na kuanza huduma. (Makofi)