Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. ASSA N. MAKANIKA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi wa Kigoma vijijini katika kukabiliana na Ugonjwa wa Mnyauko unaoharibu migomba?
Supplementary Question 1
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Ugonjwa wa mnyauko pia umekumba baadhi ya maeneo mengi ya Mkoa wa Kagera ikiwemo Jimbo la Nkenge, na mpaka sasa kwa kweli hatujapata suluhisho la ugonjwa huu na wananchi wamekata tamaa katika zao hili.
Je, ni lini sasa Serikali itatupatia ufumbuzi wa ugonjwa huu, ili tuendelee kulima ndizi kama ilivyokuwa awali? Ahsante.
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kyombo Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mikakati tuliyonayo ya kukabiliana na ugonjwa huu wa mnyauko wa migomba kwanza kabisa tumewaelekeza wakulima, kwamba pale ambapo mgomba unaonesha dalili zote za kuwa na bakteria hawa mgomba huo ung’olewe na uchomwe, ikiwa ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili tunawashirikisha kituo chetu cha utafiti cha TARI Maruku kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji wa miche bora na safi ambayo haitakuwa na changamoto ya ugonjwa huu. Tatu, kwa kutumia TARI Mikocheni lakini vilevile kilimOrgano Dar es Salaam na Crop Biosciences Solution ya Arusha tuko katika mpango wa uzalishaji wa miche kupitia Tissue Culture kuhakikisha kwamba tunakuwa na miche bora na safi ili tuondokane na tatizo hili la ugonjwa wa mnyauko wa migomba. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved