Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itafanya tathmini kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Manunuzi wa Umma ya Mwaka 2013 katika Sehemu ya 64(2)(C) ya Kanuni ya 30(c) kama ilivyofanyiwa Marekebisho?
Supplementary Question 1
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa sheria hii inataka kwenye kila manunuzi asilimia 30 ziweze kunufaisha makundi maalum ya vijana na wanawake;
Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa maelekezo mahususi kwa Maafisa Masuhuli wote nchi nzima ili waweze kufuata sheria hii? (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kila siku inayokwenda tunatoa maelekezo kwa maafisa wetu wa ununuzi; na hivi karibuni tarehe 30 Mei tulizindua kanuni maalum ambazo tumeziweka meno zitakazosaidia katika kuzingatia masuala yote ya kisheria na taratibu. Pia nachukua fursa hii kutoa maelekezo kwa maafisa masuhuli wote wa ununuzi nchini wazingatie sheria na taratibu zilizowekwa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved