Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakarabati kituo cha Polisi cha wilaya na nyumba za askari katika jimbo la Muhambwe.
Supplementary Question 1
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza nichukue nafasi hii kuwapatia pole wananchi wote wa Muhambwe kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyoibuka hivi karibuni. Hata hivyo, niishukuru Serikali kwa jitihada za haraka mbalimbali ambazo zinaichukua baada ya matukio haya kutokea. Ninayo maswali madogo ya nyongeza. (Makofi)
Je, ni lini Serikali itakarabati nyumba hizi kwa haraka, ili kuboresha ufanisi wa askari hawa?
Je, Serikali haioni iko haja ya kuongeza askari katika Jimbo hili la Muhambwe, ili kukabiliana na uhalifu huu unaotokea mara kwa mara?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hii nimpongeze sana kwa kazi nzuri anayoifanya jimboni, na pia kwa kuendelea kuwajali wananchi hasa katika sekta ya ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Naibu Spika, azma ya Serikali hii ya Mama Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi zake kwa urahisi zaidi. Ndiyo maana imeazimia kuhakikisha kwamba inaenda kujenga nyumba ama kuimarisha nyumba za makazi ya Askari Polisi, lengo na madhumuni ni Askari waweze kuishi katika mazingira mazuri. Pia tunahakikisha kwamba tunajenga vituo vizuri na vya kisasa vya Polisi ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, tunaenda kutafuta fedha ili na zitakapopatikana Jimbo la Muhambwe tutalipa kipaumbele kuwapatia vituo na nyumba za maaskari.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuendelea kujibu swali lake lingine, nimwambie tu Mheshimiwa kwamba Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan alitoa kibali cha kuajiri Askari Polisi takribani 3,000. Sasa nimwambie askari hawa sasa hivi wapo kwenye mafunzo, lakini watakapomaliza tu mafunzo tutahakikisha Muhambwe tunapeleka askari wa kutosha ili wananchi waweze kuishi katika mazingira ya ulinzi na usalama zaidi, nakushukuru. (Makofi)
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakarabati kituo cha Polisi cha wilaya na nyumba za askari katika jimbo la Muhambwe.
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo letu la Kilwa Kaskazini kuna Kituo cha Polisi cha Somanga. Kituo kile kimechakaa sana. Sijui ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Polisi Somanga?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndulane, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoanza kusema awali, azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunaboresha vituo vya Polisi vyote nchini ili wananchi waweze kupata huduma kirahisi, na pia Askari Polisi waweze kufanya kazi zao kwa muwala na utulivu zaidi kama wanavyotakiwa. Namwomba Mheshimiwa awe na subira, tunatafuta fedha. Zitakapopatikana, baada ya Muhambwe, basi na jimbo lako Mheshimiwa tutalipa kipaumbele kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved