Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TAUHIDA C. GALLOS aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika kila Kituo cha Afya nchini?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA A. MZEE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Je, ni lini Serikali itaanza huduma ya utoaji huduma ya afya kwa wazee?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwa kweli utoaji wa huduma za afya kwa wazee unaendelea. Ni kwamba tu tuhamasishane sisi Wabunge, tunapokuwa kwenye majimbo yetu kupitia Serikali ya Wilaya husika na Baraza letu la Madiwani, tushirikiane sote kwa pamoja kusimamia taratibu na kanuni za Serikali ili kila jambo ambalo limeelekezwa kwenye policy za Serikali liweze kutekelezwa ipasavyo na watendaji wetu kule chini.