Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haielimishi wananchi kujiepusha na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi hadi pale maafa yanapotokea?

Supplementary Question 1

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; pamoja na kwamba Serikali imeendelea kutoa taaluma au elimu kwa wananchi mbalimbali kwa vyombo mbalimbali, je, Serikali imefanya tathmini kujua ni kiasi gani elimu hiyo inawafikia na inawasaidia wnanchi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa sababu, Jimbo la Mwera ni jimbo la vijijini na athari kubwa inatokea kwenye mambo haya ya mazingira ambayo Mheshimiwa Waziri anasema wanatoa elimu. Je, ni lini sasa Mheshimiwa Waziri, physically, pamoja na wataalam wake wanaweza kwenda kusaidia kutoa elimu wao wenyewe? Nakushukuru sana.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la kaka yangu, Mheshimiwa Zahor, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kuweka record sawa; kaka yangu, Mheshimiwa Zahor, ni mzoefu sana, wakati anamsaidia Makamu wa Rais wakati ule alifanya kazi kubwa sana. Kwa hiyo, naomba kumpa maua yake kwa kazi kubwa aliyoifanya katika upande wa muungano na upande wa mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa tathmini, hivi karibuni tutatoa taarifa yetu ya mazingira ambapo, naamini utakapofika Mwezi Juni tutakuwa tumepata taarifa ambayo iko very comprehensive. Nina imani kwamba, baada ya taarifa hii tutaona tathmini ya hali ilivyo kwa maeneo hayo yote. Kwa hiyo, tusubiri mpaka Mwezi wa Sita, Siku ya World Environment Day, taarifa hii itatoka kwa lengo la kujua tathmini ya athari za mabadiliko ya tabianchi na athari za kimazingira kwa maeneo mbalimbali iko vipi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala zima la kutoa elimu; naomba nilichukue hili kwa sababu, nina dhamana ya Muungano. Mheshimiwa Mbunge atakumbuka huwa naenda katika majimbo yao kutembelea miradi ya Mfuko wa Jimbo na mambo mengine. Hili tunalichukua, tutaona namna bora zaidi kwa kushirikiana na wenzetu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza, kule Zanzibar, kuona jinsi tutakavyofanya ili kuwafikia wananchi wa Mwera kwa ajili ya upatikanaji wa elimu. Ahsante sana.

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haielimishi wananchi kujiepusha na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi hadi pale maafa yanapotokea?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Kata ya Sanza iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kuna Mto Sanza ambao mabadiliko ya tabianchi yamesababisha mto huo kuchepuka na kuathiri makazi na Kanisa la Roman Catholic. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba, madhara haya yanakabiliwa? Ahsante sana.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mbunge wa Manyoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, kwanza namshukuru Mheshimiwa Mbunge alikuja kunijulisha taarifa hii. Binafsi nasema kwamba, tunakiri tatizo hilo lipo, lakini kubwa zaidi sasa hivi tunaainisha maeneo yenye tatizo hilo kwa sababu yako mengi sana, tuna kule Manyoni, tuna Mpwapwa, tuna Mvomero, maeneo haya yamekithiri zaidi. Kwa hiyo, tutaangalia jinsi gani ya kufanya ili kushughulikia eneo hilo, lakini najua kweli ni tatizo kubwa, linaathiri hata lile jengo la kanisa, nalo liko hatarini Ahsante.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haielimishi wananchi kujiepusha na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi hadi pale maafa yanapotokea?

Supplementary Question 3

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Hongera sana kwa Mheshimiwa Waziri, anafanya kazi kubwa ya kutunza mazingira ya nchi yetu. Sasa athari zimetokea na katika baadhi ya maeneo wananchi wamekumbwa na mafuriko makubwa ikiwemo Jimbo la Kilombero, Halmashauri ya Mji wa Ifakara. Hivi ninavyozungumza wananchi takriban 300 wako kambini katika shule. Je, Serikali na Ofisi ya Waziri kwa kushirikana wananisaidiaje kupata chakula cha dharura kwa wananchi wangu wa Jimbo la Kilombero?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Comrade, Mheshimiwa Asenga, Mbunge wa Ifakara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna maeneo sasa hivi yana athari kubwa sana, kuna eneo la Ifakara, Rufiji na maeneo mbalimbali. Kwa kweli, athari ya mafuriko imekuwa ni kubwa sana. Juzi nilikuwa naongea na moja ya balozi kwa ajili ya kuona jinsi wanavyoweza kusaidia na wameanza kutoa timu kupeleka katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu jambo hili ni jambo la kiutu zaidi, nawaomba wadau mbalimbali hasa wa kimaendeleo wabaini kwamba, watu sasa hivi wanaathirika, wawafikie ili kuwapa msaada kwa sababu kweli limekuwa ni tatizo kubwa na maeneo mbalimbali yanaathirika. Hoja ya Mheshimiwa Mbunge imechukuliwa na Serikali itaitafakari kwa upana zaidi. (Makofi)

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haielimishi wananchi kujiepusha na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi hadi pale maafa yanapotokea?

Supplementary Question 4

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Vikundi vingi vya mazingira vimekuwa vikikosa motisha na uwezo. Je, Serikali inachukua hatua zipi kuvijengea uwezo?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Comrade, Mheshimiwa Mchungahela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, kuna vikundi vingi ambavyo vimejihamasisha zaidi kuhakikisha vinashughulika na shughuli za kimazingira, lakini wakati mwingine vinakuwa na changamoto ya bajeti. Nachukua fursa hii kuomba Mamlaka za Serikali za Mitaa, kupitia dirisha la utoaji wa fedha kwa ajili ya vikundi, ziangalie kama kuna vikundi vya kimazingira ambavyo vinaweza kupatiwa mtaji wa uzalishaji wa miti waweze kufanya hivyo, kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vyetu mbalimbali kuwa na nguvu na uwezo kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kimazingira.