Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO K.n.y. MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:- Je, mikopo kiasi gani imetolewa na Taasisi za Fedha kwa dhamana ya mali zilizorasimishwa na wanawake wangapi wamenufaika?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuweza kuuliza swali dogo la nyongeza. Benki zetu bado riba ni kubwa sana. Je, Serikali haina mpango wa kufikiria kupunguza riba ili angalau wananchi walio wengi waweze kukopa katika benki zetu?
Name
Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Magharibi
Answer
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iko kwenye mpango huo na jambo hilo linalohusisha riba ni jambo mtambuka, lina hatua nyingi mpaka kufikia kwenye hatua hiyo. Moja ya hatua ambayo Serikali imefanya, umeona kwenye masuala ya sensa na makazi, masuala ya vitambulisho vya Taifa, hayo yote ni ya kuwezesha wananchi watambulike ili kupunguza risk na risk zikipungua, definitely tutakuwa tunaenda kwenye uelekeo huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea pia kuongea na Benki Kuu pamoja na benki zingine, kuweza kuona utekelezaji wake ili uweze kufanyika bila kuathiri sekta ya fedha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved