Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, upi mpango wa kuwasaidia wakulima wa tumbaku kupata vitendea kazi mapema na kupunguza bei vikiwemo Jute Twine na Cotton Twine?
Supplementary Question 1
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake, lakini nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba wakulima wa tumbaku nao wanapata mbolea ya ruzuku? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; wako wakulima wa tumbaku ambao waliuza tumbaku yao tangu kipindi cha kilimo mwaka 2021. Wameuza tumbaku yao mpaka leo hawajalipwa na wanawadai walionunua zaidi ya shilingi milioni 72. Je, Serikali inawasaidiaje wakulima wa tumbaku wa Urambo ambao jambo hili linawakwaza sana? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mama Samwel Sitta kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu madai ya wakulima wa msimu wa 2019/2020 ambapo ni kama jumla ya dola milioni tano kwa Sekta nzima. Nataka tu kumhakikishia cha kwanza Serikali imefutia hizi Kampuni zote ununuzi na ushiriki kwenye Sekta ya Tumbaku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; Serikali sasa hivi tuko kwenye hatua za mwisho kuwapeleka Mahakamani kwa ajili ya madai haya ya wakulima. Pia, tunawapeleka Mahakamani pamoja na Wakurugenzi at a personal capacity kwa sababu walikuwa ni guarantor kwenye biashara hii. Kwa hiyo nataka nimhakikishie kwamba Serikali imeendelea kuchukua hatua katika hili na mwaka uliofuata mpaka sasa Kampuni yoyote ambayo imekuwa ikichelewesha malipo ya wakulima tumekuwa hatuiruhusu kuendelea kuwepo katika Sekta ya Tumbaku kwa hiyo tunaendelea kuboresha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie na ni wahakikishe wakulima wa tumbaku kwamba sasa hivi tumeamua kuwapeleka mahakamani hawa wafanyabiashara na tutachukua hatua ili tuweze ku-recover fedha za wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ruzuku nataka tu niwahakikishie wakulima wa tumbaku. Katika bajeti yetu mliyotupitishia Waheshimiwa Wabunge mwaka huu, zao la tumbaku tumeliweka kuwa moja ya zao ambalo tunalipatia ruzuku katika uzalishaji kuanzia mwaka ujao wa fedha. Kwa sababu mwaka huu wakulima wa tumbaku wamepata tatizo la mvua nyingi, uzalishaji kwa maana ya quantity haijaathirika lakini ubora wa tumbaku kidogo umeshuka kwa sababu ya mvua nyingi. Serikali imeamua kwamba zao la tumbaku litakuwa sehemu ya subsidy scheme kwenye NPK 10-18-24 yenye thamani ya shilingi bilioni 13 ili kuweza kushusha gharama zao za uzalishaji. (Makofi)
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, upi mpango wa kuwasaidia wakulima wa tumbaku kupata vitendea kazi mapema na kupunguza bei vikiwemo Jute Twine na Cotton Twine?
Supplementary Question 2
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa bei za zao la tumbaku mwaka huu zinaonekana ziko chini sana baada ya zao la tumbaku kukumbwa na tatizo la mvua nyingi. Serikali ina mkakati gani wa kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji ambazo zimewalazimu mwaka huu watumie pembejeo mara mbili ya kile kiwango kinachotakiwa, Serikali wanatusaidiaje wakulima wa tumbaku?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani narudia tena jibu nililojibu kwenye swali la Mheshimiwa Margaret Sitta. Ni kwamba baada ya kuona hali ya mvua na gharama za uzalishaji na wakulima wametumia pembejeo zaidi ya mara moja au mara mbili mwaka huu ili kulinda zao la tumbaku. Serikali itatoa ruzuku ya shilingi bilioni 13 kwenye gharama za uzalishaji kwa wakulima wa tumbaku katika mwaka huu wa fedha ambao tunaendelea nao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaanza kukusanya takwimu kupitia Vyama vyao vya Ushirika na Bodi ya Tumbaku ili kuweza kuwapunguzia gharama, kwa sababu tusipofanya hivyo wanaweza wakapata hasara na kuwavunja moyo kwa sababu sasa hivi kwa jitihada walizofanya wakulima Tanzania imekua ni nchi ya pili ya uzalishaji wa tumbaku Afrika kutoka nchi ya tano. (Makofi)
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Je, upi mpango wa kuwasaidia wakulima wa tumbaku kupata vitendea kazi mapema na kupunguza bei vikiwemo Jute Twine na Cotton Twine?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatafutia soko la uhakika wakulima wa mazao ya viungo katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ishengoma kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja; mazao ya spice yalikuwa hayajawekwa katika utaratibu mzuri na kuya-categorize katika eneo gani la mazao. Serikali ilichukua hatua ya kuyaweka katika mazao mbayo yanatazamwa kama ni mazao ya horticulture; kwa hiyo hilo la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Serikali imechukua hatua kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ithibati ya Kimataifa ili mazao yetu yaweze kufunguliwa katika masoko mbalimbali. Nataka niwape taarifa kwamba sasa hivi mazao yetu ya viungo yamepata ithibati ya kuwa miongoni mwa mazao ambayo ni organic katika Soko la Dunia na yameanza kutoka kwenda maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, kama Serikali ili kuweza kuwasaidia wakulima wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Tanga wa mazao ya viungo. Serikali imechukua hatua ya kukigeuza Kituo chetu cha Utafiti cha Tanga kuwa Center of Excellency kwa ajili ya spice. Kwa hiyo na yenyewe nayo tumeyaweka katika ramani kama mazao muhimu ya export na tunaendelea kufanya jitihada. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved