Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Adamson Mwakasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza tatizo la mtandao wa simu kwenye baadhi ya maeneo katika Jimbo la Tabora Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nianze kwa kuipongeza Serikali, hasa kwa kuboresha mitandao ya mawasiliano katika Jimbo langu la Tabora Mjini. Pamoja na hayo nina swali moja tu la nyongeza. Kata ya Malolo, maeneo ya wafugaji, maeneo ya Usenge, pia na Kata ya Ikomwa, pamoja na Kata ya Ntalikwa bado kuna matatizo makubwa ya mawasiliano, sijui Serikali…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Waheshimiwa Wabunge hivyo ndivyo jina linavyoitwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo makubwa ya mawasiliano.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha mawasiliano katika maeneo hayo?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyoeleza, Kata ya Malolo eneo la Usenge, Kata ya Ikomwa na Ntalikwa kuna matatizo ya mawasiliano. Nawaagiza TCRA na UCSAF baada ya bajeti yetu kupita kesho waende maeneo hayo, wafanye tathmini, walete ripoti ili tufanye uamuzi wa kupeleka mawasiliano. (Makofi)
Name
Khalifa Mohammed Issa
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Mtambwe
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza tatizo la mtandao wa simu kwenye baadhi ya maeneo katika Jimbo la Tabora Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Maeneo makubwa ya Jimbo langu la Mtambwe, Pemba yana shida ya mtandao wa simu. Je, ni lini Serikali itatatua tatizo hili?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imejenga minara 48 katika Visiwa vya Pemba na Unguja kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano. Tumepeleka mpaka kwenye visiwa ambako wananchi wanafanya shughuli zao za uvuvi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokea pia ombi la Mheshimiwa Mbunge kwamba, kama kuna maeneo ambayo bado yana tatizo tutakuja kufanya tathmini baada ya hii miradi ya minara 48. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunayo minara mingine, tutaiongeza kwenye maeneo yale ambayo bado yana changamoto ya mawasiliano. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved