Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amina Ali Mzee
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza wimbi la vijana wanaomaliza masomo na kukosa kazi kutokana na sharti la vigezo vya uzoefu wa miaka miwili na zaidi?
Supplementary Question 1
MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia maboresho ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, ni upi mkakati wa Serikali kuongeza ajira kwa vijana nchini? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia maboresho yaliyofanyika ya Sera ya Maendeleo ya Vijana, katika moja ya kitu kikubwa ambacho kimefanyika, kwanza ni kutambua vijana wenyewe ni akina nani.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kutambua vijana katika kila eneo la sekta ya kuzalisha ya kiuchumi na kimaendeleo kwa nchi yetu. Katika kufanya hivyo pia ndani ya Sera ya Vijana, moja ya kitu kikubwa ambacho kimeongezwa sasa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na programu za malezi ili kumsaidia kijana huyu siyo tu ajiandae kuajiriwa ndani ya Serikali, lakini pia kumuwezesha hata kiuchumi, kifedha ili aweze kujiajiri mwenyewe na kuweza kujitegemea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndani ya sera hiyo yapo maboresho makubwa mengi yaliyofanyika, lakini kubwa kuliko lote ni lile sasa la kutambua vijana katika kila sekta ya kimaendeleo. (Makofi)
Name
Janejelly Ntate James
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza wimbi la vijana wanaomaliza masomo na kukosa kazi kutokana na sharti la vigezo vya uzoefu wa miaka miwili na zaidi?
Supplementary Question 2
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na juhudi nzuri sana za Serikali kwa jinsi mnavyowaangalia vijana, je, sasa Serikali hamjaona kuna umuhimu wa kuchukua vijana kwa taaluma zao, kuwapanga pamoja na kutumia mikopo ya halmashauri mkisaidiana na TAMISEMI ili kuwapa hiyo mikopo waitumie kujiendeleza kitaaluma bila kutegemea ajira za Serikali? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, maelezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Mbunge kwanza ninakiri kuyachukua kama ni ushauri mzuri, lakini ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba vijana wanawezeshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya jambo kubwa inalofanya ni kuwawezesha vijana katika ujuzi ambapo programu mbalimbali ikiwemo Programu ya Uanagenzi nayo ni moja katika jambo kubwa ambalo linafanyika ndani ya Serikali ili kuwawezesha vijana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako kwamba Serikali itaendelea kuyafanyia kazi kuhakikisha kwamba tunawezesha vijana kwa sababu ukiwezesha vijana ndiyo umewezesha nguvu ya Taifa. (Makofi)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, kuna mradi Bangladesh wamezindua unaitwa Decentralization and Eligible Energy. Mradi huu unasaidia vijana wengi kuingia katika biashara hii, kupeleka umeme huu wa nishati ya jua kwenye vijiji vingi na wengi walijipatia ajira. Nendeni Bangladesh mkajifunze muone namna gani mtasaidia vijana wa Kitanzania. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved