Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa ghala la mazao Wilayani Tunduru lililoanza kujengwa na Bodi ya Korosho mwaka 2014?

Supplementary Question 1

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru kwa majibu mazuri, lakini nilikuwa namwomba Waziri alete muda specific ni lini mchakato huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani ni muhimu sana kuwa na maghala ya kisasa hasa kwenye maeneo ya vijiji. Ni nini mkakati wa Serikali kujenga maghala katika vijiji mbalimbali vilivyopo katika Jimbo la Tunduru Kusini? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mpakate, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini utakamilika.

Mheshimiwa Naini Spika, siwezi kusema lini utakamilika wakati hata kurudi site hatujarudi. Tumerudisha mfuko pamoja na ninalishukuru Bunge lako Tukufu Mfuko wa Kuendeleza Zao la Korosho ulikuwa umefutwa sasa tunaanza kupata fedha na nimesema katika bajeti ya mwaka huu 2024/2025 tumetenga fedha kwa ajili kuanza kujenga maghala haya yote matatu ambayo yalikuwa yamesimama toka mwaka 2015.

Kwa hiyo, ni matarijio ya Serikali kwamba ndani ya mwaka huu wa fedha wakandarasi watarudi site kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu maghala ya vijijini, nataka nimuombe tu Mheshimiwa Mbunge hata kwenye kikao cha wadau wa korosho tulijadili, Serikali inaendelea kujenga maghala vijijini kila mwaka lakini jambo la misingi ambalo tunalifanya sasa hivi, kwanza ni kufanya audit ya maghala yaliyojengwa na Serikali ambayo yamebaki vijijini yamekuwa idle ili kuweza kuyatumia na kuyarasimisha rasmi na kufanyia rehabilitation. Mkoa wake tu katika mwaka wa fedha uliopita tumejenga maghala zaidi ya 28 ingawa Jimbo lake halikupata katika hayo maghala.

Kwa hiyo, nimhakikishie ni mpango wa Serikali kuendelea kujenga maghala vijijini ili kuondoa tatizo la stakabadhi ya ghala, lakini vilevile matatizo ya uhifadhi wa mazao ya wakulima.

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa ghala la mazao Wilayani Tunduru lililoanza kujengwa na Bodi ya Korosho mwaka 2014?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naipongeza Serikali kwa kuanza utekelezaji mradi wa kongani ya viwanda vya korosho pale Malanje na kuna ujenzi wa maghala mawili umeshaanza, lakini kwa ramani ya pale tumeona kwamba kutakuwa na ujenzi wa maghala 10.

Je, Wizara ina mpango gani wa kupeleka fedha nyingine za ujenzi wa maghala nane yaliyobaki? Nakushukuru.

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimuombe Mheshimiwa Chikota, Mbunge wa Nanyamba jambo moja; kwanza, tukamilishe mradi ambao tumeuanza, halafu tutafanya miradi mingine baada ya kukamilisha mradi ambao tumeanza hivi sasa. Ni mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba Malanje Industrial Park inakamilika na private sector wameanza kuja tutawahusisha na wenyewe katika ujenzi wa maghala.