Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo Wilayani Ileje?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza halmashauri nyingi hazina uwezo wa kujijengea viwanja zenyewe ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, sasa nataka kujua mpango wa Serikali ni upi kuhakikisha mnazishawishi taasisi binafsi ili zije ziwekeze uwanja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje hasa ukizingatia kwamba Ileje ni Wilaya ambayo ipo mpakani baina ya Malawi na Tanzania. Je, hamuoni jambo hili linaweza kuwa ni fursa?

Swali langu la pili, Halmashauri ya Mji wa Tunduma imetenga viwanja kwa ajili ya michezo kikiwepo kiwanja cha Kata ya Chapa katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma. Nataka kujua, Serikali hamuoni umuhimu wa kuharakisha zoezi hili ili uwanja uweze kujengwa na wananchi waweze kunufaika kama ilivyopagwa?

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru Mheshimiwa Stella kwa maswali yake mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali, Wizara yenye dhamana ya utamaduni, Sanaa na michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI tupo katika mkakati wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na sports centre moja katika kila halmashauri ikijumuisha viwanja au michezo yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, makakati huu utakapokamilika tutaweza kuuleta katika bajeti ya mwakani na unaweza ukaanza kutekelezwa kwa Serikali kushirikiana na taasisi binafsi na wadau wa maendeleo.

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo Wilayani Ileje?

Supplementary Question 2

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafsai ya kuweza kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametaja juhudi iliyofanywa na Halmashauri ya Manispaa pale Kinondoni ambapo jumla ya shilingi bilioni 10.1 zitatumika uwanja ule ukiwa umekamilika. Ni uwanja wa mfano mpaka Simba Sports Club inakwenda kucheza pale.

Sasa Mheshimiwa Waziri, ningekuomba uipongeze Halmashauri ya Manispaa kisawa sawa, halmashauri inayoongozwa na Mstahiki Meya Songoro Mnyonge, Naibu Meya Michael Urio pamoja na Mkurugenzi Hanifa Hamza na Mbunge wao Tarimba Abbas.

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie tena. Nichukue nafasi hii kuipongeza Halmashauri ya Kinondoni inayoongozwa na Mheshimiwa Mbunge Abbas Gulam Tarimba kwa kujenga uwanja mzuri wa kisasa ambao umetumika kwenye mashindano ya CECAFA na sasa hivi unatumika na vilabu vyetu vikubwa vya Simba na Yanga. Halmashauri nyingine tuige mfano Halmashauri ya Kinondoni. (Makofi)

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo Wilayani Ileje?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, ni kwa nini Serikali isiweke kipaumbele cha ujenzi wa uwanja wa kisasa Wilayani Butiama ambapo ni kwa Baba wa Taifa katika kumuenzi ili kiweze kutumika kwenye mashindano ya AFCON na kuweza kutoa fursa kwa watu wengi kutembelea hata kaburi la Baba wa Taifa na kukuza utalii? (Makofi)

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Answer

WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirejee tena, jukumu la msingi na la awali ni la halmashauri husika na ndiyo maana nimezipongeza halmashauri ambazo zimefanya vizuri ikiwemo Halmashauri ya Ruangwa ambayo inaongozwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa kujenga uwanja mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara na Serikali tutashirikiana na halmashauri ya Butiama kuwapa ushauri na kuwatafutia wadau ili wafanye kama halmashauri hizi nyingine ya Ruangwa, Kinondoni, Nyamagana, Babati na halmashauri nyingine. (Makofi)