Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya lami kutoka Choma - Ziba na Ziba - Puge utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri mwaka jana katika bajeti ilikuwa ya 2023/2024 tulitengewa kilometa kumi na mwaka huu wa fedha tulikuwa tumetengewa kilometa nyingine. Tulitarajia katika kutangaza zabuni kilometa zaidi ya 22 ziweze kutangazwa. Je, mtazingatia hilo Mheshimiwa Waziri? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu langu kwamba tutaanza hizo kilometa 11, lakini kama hali ya bajeti tutapata fedha tutaendelea kuijenga na lengo si kujenga hii barabara tu kwa awamu, lakini tukiweza kupata hela nyingi zaidi tuna uwezo wa kuijenga hiyo barabara yote, lakini kwa sasa tutaanza na hizo kilometa 11, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved