Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu - Morogoro MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na nashukuru sana kwa majibu ya Serikali ambayo ni mazuri, hata hivyo naomba sana hizi zahanati zikarabatiwe haraka kwa sababu Kituo cha Afya Mzinga ni cha kulipia.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, Kituo cha Afya Mafiga nimekuwa nakiulizia humu mara kwa mara ni kituo ambacho kinapendwa na akinamama kwenda kujifungulia, lakini bahati mbaya mpaka sasa hivi hakina jengo la upasuaji kwa sababu wakipata matatizo wanakwenda kwenye hospitali kubwa. Kwa hiyo, ni lini jengo hili la upasuaji litajengwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, Kituo cha Afya cha Lumuma bado hakijajegwa na huko huko kuna wananchi wengi ambao wanalima vitunguu na wanapaswa kwenda kutibiwa kwenye Wilaya ya Mpwapwa ambayo ipo kwenye Mkoa wa Dodoma. Je, ni lini hiki Kituo cha Afya Lumuma kitajegwa? Ahsante sana.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Mama Ishengoma amefuatilia mara kadhaa lakini nipokee maoni yake na hoja zake kuhusiana na ukarabati na upanuzi wa zahanati hizi za Magadu na Mgambazi na nimhakikishie kwamba Serikali imeshaanza kutenga fedha ili kuboresha zahanati hizo ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Kituo cha Afya cha Mafiga ni kweli kituo kile ni miongoni mwa vituo vikongwe 202 ambavyo tumeshaviainisha, tunakamilisha ukarabati wa hospitali za halmashauri kongwe 51, tumeshakarabati 32 bado 19, tukishakamilisha 19 za halmashauri tunakwenda kwenye vituo vya afya 202 kikiwemo Kituo cha Afya cha Mafiga ambacho kitajengewa wodi pamoja na jengo la upasuaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kituo cha afya katika Kata ya Lumuma nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kata zote zenye idadi kubwa ya wananchi na umbali mkubwa kutoka kituo cha karibu zaidi cha huduma zimewekwa kipaumbele kama kata za kimkakati na tutatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, ahsante.

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu - Morogoro MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro?

Supplementary Question 2

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Kituo cha Afya cha Tarakea kitaboreshwa ili kiweze kutoa huduma ya upasuaji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba nichukue hoja ya Mheshimiwa Mbunge, amefuatilia mara kadhaa na sisi kama Serikali kazi yetu ni kupokea maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge kwa ajili ya kwenda kutengeneza mipango na bajeti kwa ajili ya ukarabati. Kwa hiyo, Kituo cha Afya cha Tarakea tumekichukua Mheshimiwa Mbunge, tutakiwekea mpango kwa ajili ya ukarabati. (Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

Ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu - Morogoro MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, je, kati ya hivi vituo vikongwe vya afya 200 ambavyo umetaja kwamba viko kwenye mchakato wa kukarabatiwa unaweza ukanihakikishia kwamba Kituo cha Mwika Msae kiko katika hivi 200?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, vituo vya afya 202 vilifanyiwa tathmini ya kuonekana ni vituo chakavu zaidi, sasa kwa sababu Mheshimiwa Mbunge Dkt. Kimei angependa kujua kama Mwika imo, naomba baada ya kipindi hiki cha maswali na majibu nirudi kwenye records zetu na nitakufuata hapo Mheshimiwa nikupe kama ipo halafu twende kwenye hatua nyingine. (Makofi)

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

Ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu - Morogoro MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Magadu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro?

Supplementary Question 4

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kinondoni imetumia takribani fedha za Mfuko wa Jimbo shilingi milioni 129 kujenga kituo cha mionzi (x-rays pamoja na ultra sound). Serikali imeweza kutupatia vifaa kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kituo kile kinafanya kazi.

Je, Serikali iko tayari kupokea pongezi za wananchi wa Kinondoni kwa msaada mkubwa waliotupatia juu ya vifaa vile na sasa kituo kile kinawasaidia wananchi wa Jimbo la Kinondoni?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Tarimba kwa kutoa fedha hizo shilingi milioni 129 kujenga jengo la mionzi katika vituo vyake katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na pongezi hizo tunazipokea na zimwendee Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapenzi yake makubwa kwa wananchi na ndio maana huduma za afya zinaendelea kuimarika Kinondoni na kote nchini, ahsante.