Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
Hitaji la Posho za Kujikimu kwa Wafanyakazi Wanaojitolea MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:- Je, kwa nini Serikali isiwalipe posho sawa ya kujikimu wafanyakazi wanaojitolea ili kuondoa matabaka ya malipo kulingana na sehemu wanazofanya kazi?
Supplementary Question 1
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini tumekuwa tukiona taasisi mbalimbali kwa mfano TRA, Benki Kuu, Bandari na taasisi nyingine mbalimbali ambazo zinawapa vijana nafasi za kujitolea, lakini hakuna utaratibu maalumu ambao umewekwa wa kujua kwamba hawa vijana wanaenda kupata hizo nafasi namna gani na hii inaweza ikatokea ama boss ama mfanyakazi akaweza kumpa nafasi hiyo matokeo yake tunavyokuwa tunaomba vijana hawa wapate ajira kwa sababu wamejitolea unakuta unaweka mlolongo wa walewale ambao wako katika ofisi hiyo.
Sasa swali langu hapa, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba mna utaratibu maalumu wa kuwapata vijana wanaojitolea katika taasisi mbalimbali hata Serikalini?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pamoja na kusema kwamba kuna mwongozo au taratibu ambazo mmeziweka, ni lini sasa mwongozo huu utatoka hara ili vijana wetu waweze kupata nafasi hizo? Ahsante.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Grace Tendega, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa akiwasemea vijana wa kitanzania hasa awale ambao wamekuwa wakijitolea amepaza sauti sana kuwasemea.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu maswali mawili yake ya nyongeza kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba Serikali inatambua na baada ya kuona changamoto hiyo hasa katika taasisi mbalimbali kwa namna ambavyo wanawapata vijana wa kujitolea. Tuko mbioni tunaandaa randama ambayo baada ya kukamilika tutatoa waraka namna na utaratibu wa kuwapata vijana hawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee Serikali imeona kwamba itaweka utaratibu wa ushindani ilikijana aende kujitolea sehemu tunaenda kuweka utaratibu kama tunavyofanya kwenye ajira za sasa ambazo zimetangazwa kwenye kada ya ualimu, kada ya afya na kada nyinginezo. Kwa hiyo, nimuondolee shaka Mheshimiwa Mbunge, Serikali inalitambua hilo na ndio maana imeingia kwenye mchakato huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lini tutatoa waraka huo, naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa fedha tayari waraka huu utakuwa umetoka kuwaongoza Wakuu wa Taasisi namna ya kuwapata vijana wa kujitolea, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved