Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Adamson Mwakasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuimarisha upatikanaji wa mtandao wa simu katika kata 29 za Tabora Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Jimbo la Tabora Mjini lenye kata 29 bado kuna kata ambazo zina matatizo sana ya mawasiliano katika baadhi ya maeneo, kwa mfano, ukienda Kata ya Ndevelwa kuna maeneo ambayo huwezi kabisa kupata mawasiliano. Ukienda Kata ya Ikomwa na hata hiyo Kata ya Itetemya, tena karibu na mjini kabisa, kuna maeneo kama yale ya Kipalapala pale ambapo kuna mission bado kuna shida ya mtandao na maeneo mengine.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha yale maeneo yote ya Tabora Mjini ambayo hayafikiwi na mawasiliano yatafikiwa na hayo mawasiliano? Hilo la kwanza.
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kata ya Kiloleni ambayo iko kwenye majibu ya Mheshimiwa Waziri iko center kabisa ya Mji wa Tabora kwa maana ipo mjini pale pale. Sasa pengine niwashauri tu, nilikuwa na ombi, kwa kuwa pale Kiloleni hakuna shida kabisa ya mawasiliano ni mjini kabisa, kwa nini huo mtambo ambao mtaupeleka pale katika Kata ya Kiloleni ambayo iko mjini kabisa msipeleke maeneo ambayo bado kuna shida ya mawasiliano?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kama nilivyoeleza kwenye jibu langu la msingi, tayari kuna jitihada zinafanyika na tutazisimamia kuhakikisha mawasiliano yanaimarika katika maeneo haya ya Jimbo la Tabora Mjini.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kuhamisha mtambo kutoka Kiloleni kwenda eneo alilolitaja Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Serikali tuko tayari kushauriana naye na baada ya hapa tuonane ili tuweze kuona namna njema ya kufanya katika hili.
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuimarisha upatikanaji wa mtandao wa simu katika kata 29 za Tabora Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniruhusu niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Tabora Kaskazini, kata mbili ambazo ni Kata ya Igulungu, Kijiji cha Mbeya ambako kuna zahanati hakuna kabisa mawasiliano, lakini pia Kata ya Ibiri hakuna mawasiliano; je, ni lini Serikali itajenga minara katika kata hizo mbili? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Almas Maige, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika kata hizi mbili jana tuliongea na Mheshimiwa Maige na tayari watendaji wanashughulikia. Katika mwaka ujao wa fedha tutafanya baadhi ya maeneo ili kuhakikisha mawasiliano yanakaa vizuri.
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuimarisha upatikanaji wa mtandao wa simu katika kata 29 za Tabora Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali ilipeleka Kampuni ya TTCL kupitia UCSAF kwenda kujenga minara miwili katika Kijiji cha Mtelawamwahi na Kijiji cha Mdwema, lakini tangu walipokwenda mpaka leo hawajurudi kujenga hiyo minara; je, Serikali inaweza kuhimiza Kampuni ya TTCL kujenga hiyo minara ya Mdwema na Mtelwamwahi?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa kuwa katika vijiji hivi tutafutailia kwa karibu na ikiwezekana tutakwenda kufanya ziara ili kuona ni kwa nini minara hii haijajengwa na lengo ni kuona wananchi wanapata mawasiliano ya uhakika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved