Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bonnah Ladislaus Kamoli
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Segerea
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, ni kweli kauli ya Serikali kwa hospitali kutozuia maiti kwa sababu ya deni la matibabu ni ya kisiasa?
Supplementary Question 1
MHE. BONNAH L. KAMOLI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri aliyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado hata kwenye mikoa yetu na wilaya mbalimbali bado watu wanazuiwa maiti zao na sisi kama wawakilishi wa wananchi huwa tunapigiwa simu kuhusiana na hili suala la kuzuia maiti.
Kwa hiyo, nilikuwa namuomba Mheshimiwa Waziri pamoja na majibu yake aliyosema kwamba sasa hivi wametoa mwongozo naomba hao watu wazingatie mwongozo.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ili watu hawa ambao wanapoteza wapendwa wao badala ya kuanza kuzuiwa kwamba wasichukue watu wao, je, kwa nini sasa Serikali isiweze kuimarisha Bima ya Afya ili hawa watu wakapewa mwili wao kwa sababu wanakuwa wamepata matatizo? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kweli ni Mbunge ambaye amekuwa akishirikiana na Wizara ya Afya kwa masuala mbalimbali yanayohusu afya kwenye wilaya yake ambayo anaisimamia.
Mheshimiwa Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge tutakachokifanya nitumie tena hii fursa kuwambia Waganga Wafawidhi, Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya zetu na wataalamu wote wa afya wahakikishe huu mwongozo wanaufuata, lakini niwaombe Wakurugenzi wanaohusika na Idara ya Tiba kwenye Wizara yetu kuanzia leo waanze kushuka chini na kuanza kufanya declamation ya waraka huu ili watu wengi na wataalamu wengi wajue kwamba kuna huu waraka ili waweze kuuzingatia.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ilikuwa ni Bima ya Afya, hili la Bima ya Afya ninyi wenyewe mmeshatusaidia tumepitisha Muswada wa Bima ya Afya kwa wote nikuombe Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wenzangu tutakapoanza tuhamasishe kwa pamoja wananchi kwa sababu ndilo kweli suluhisho la kumaliza tatizo hili.
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, ni kweli kauli ya Serikali kwa hospitali kutozuia maiti kwa sababu ya deni la matibabu ni ya kisiasa?
Supplementary Question 2
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nashukuru, pamoja na Serikali kuendelea kutoa kauli kuhusiana na kutozuiliwa kwa maiti kwenye vituo vya afya na hospitali mbalimbali nchini, lakini hii imekuwa ni changamoto kubwa maeneo mengi na hii inaonekana kauli ya Mawaziri na Serikali haizingatiwi.
Sasa nataka kujua mpango wa Serikali ni upi kutoa kauli yenye ukali zaidi ili kauli zao ziweze kutekelezeka huko kwenye maeneo ya hospitalini na vituo vya afya?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza mimi naamini nimtoe tu wasiwasi Mbunge kauli za Serikali zinasikilizwa ila mtu akishafariki hospitalini haikufanyi automatically kwamba hutakiwi kulipia, ila kuna process za kuzingatia ili kuhakikisha kweli huyu ni yule asiyeweza kulipia au huyu ni wa kupewa utaratibu maalum kuhakikisha anamaliza hili deni, lakini tukubaliane hakuna kanisa wala msikiti uliouaga shetani, shetani bado yupo anatusumbua na kuna baadhi ya watendaji ambao si wasikivu tutaendelea kupambana nao pamoja na ninyi.
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:- Je, ni kweli kauli ya Serikali kwa hospitali kutozuia maiti kwa sababu ya deni la matibabu ni ya kisiasa?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi ambao hata kulipia huduma za matibabu wanakuwa hawana, lakini mgonjwa anapofariki wamekuwa hawana uwezo kabisa kwa mfano wiki iliyopita tu kuna maiti ilitoka Muhimbili watu walikuwa wanashindwa kujichangisha mpaka maiti ikachelewa kupelekwa kuzikwa. Ni kwa nini sasa hawa wasifutiwe tu maana yake waliambiwa kwamba watakapozika waende wakalipe zile gharama wanakuwa wanapata usongo wa mawazo mpaka hata afya ya akili inakuwa inawazidi? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge, lakini niendelee kusisitiza kuna utaratibu, moja; mwananchi anapotoka na anajua kwamba hawezi kulipa matibabu kwenye eneo husika washirikiane na Mwenyekiti wa Kijiji husika pamoja na Mtendaji Kata ili anapokwenda hospitali awe tayari hata kama akiwa hospitali hizo process ziendelee ili awe na barua yake kutoka Ofisi ya Kata ambayo inamthibitisha kwamba hana uwezo wa kulipa.
Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge ninyi wote hapa ni mashahidi, hata wakati mwingine japo siyo utaratibu ambao ningependa kwa sababu wengi hawawezi kutufikia, lakini ninyi Wabunge ni mashahidi mkileta kwetu matatizo ambayo kuna wananchi ambao wameshindwa kulipia tumekuwa tukihakikisha yanatatuliwa, lakini ili kutokulazimisha wakati wote Wabunge msumbuliwe hebu tuendelee kuwaelimisha wananchi kwamba kuna watendaji wetu wa kata wakipatikana barua basi mwananchi huyo automatically anasaidiwa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved