Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri. Licha ya majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili madogo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wachimbaji hawa wamefanya kazi hii ya uchimbaji kwa muda mrefu (kwa miaka mingi) kwa shida. Je, haya majibu mazuri uliyoyatoa mpango huu utatekeleza lini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa hawa wachimbaji wadogo wengine tayari wana leseni kwenye vitalu hivyo wanavyochimba kwa shida. Je, kuna mpango gani wa Serikali wa kuwaunganisha na wawekezaji ili waweze kufanya uchimbaji wa ubia? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji tumekwisha kuanza utekelezaji wa mpango huu ambao nimeuainisha tayari mwaka 2022 timu ya GST ilitumwa kwa ajili ya kufanya utafiti. Utafiti ule ulikamilika na ukawasilishwa katika ofisi za wilaya ambayo pia imeainisha maeneo ambayo yana sehemu rafiki ya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo. Pia zoezi la utoaji wa leseni linaendelea na kuwaunganisha pia na Benki na Taasisi za fedha kazi hii inaendelea. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba siyo kwamba tunategemea kuanza inaendelea hivi sasa na wachimbaji wa Wilaya ya Ulanga pia watanufaika katika hili.

Mheshimiwa Spika, la pili la kuhusu kuwatafutia wachimbaji hawa wawekezaji; kwa mujibu wa Sheria ya Madini Kifungu cha 8(3) kimeeleza wazi na kimetoa nafasi ya wachimbaji wadogo kupata msaada wa kiufundi pale ambapo wanaweza kuwapata wawekezaji wa kuingia nao makubaliano. Sisi kama Wizara tutaendelea kuwasimamia wachimbaji wadogo ili waweze kupata msaada huu wa kiufundi na waongeze tija katika uzalishaji wao sambamba na hilo pia tumekuwa tukifanya mikutano mbalimbali na safari mbalimbali za nje ya nchi kuwakutanisha na wawekezaji wakubwa ambao wanaweza kuingia nao ubia kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji wao.

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga?

Supplementary Question 2

MHE. SABASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, nini kauli ya Serikali katika kutatua mgogoro wa muda mrefu wa Kikundi cha Kagera dhidi ya Serikali ya Kijiji cha Dirifu katika Manispaa ya Mpanda?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, mgogoro huo naufahamu na nataka nimwahidi Mheshimiwa Mbunge nitakwenda mwenyewe kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro huo. (Makofi)

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga?

Supplementary Question 3

MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Shirika la STAMICO ndio walezi wa wachimbaji wadogo huku, nafikiri shirika lina jukumu kubwa la kufanya biashara. Ni lini sasa hawa wachimbaji wadogo watakuwa na kurugenzi yao inayowasimamia kuhakikisha kwamba wanaweza kufanya shughuli zao vizuri? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge chini ya Ofisi ya Kamishna kipo kitengo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambao wanasimamia na kuwashughulikia wachimbaji wadogo. Kazi ambayo wanaifanya STAMICO ni kazi ya ulezi ambayo pia imesaidia sana hasa kuboresha uchimbaji mdogo hapa nchini Tanzania. Kwa hiyo vyote viwili hivi vinafanya kazi kwa pamoja na ndiyo maana tunaona wachimbaji wadogo wameendelea kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu la Tanzania kupitia sekta ya madini kwa sababu ya ushirikiano wa maeneo haya mawili ya Ofisi ya Kamishna pamoja na STAMICO kama mlezi.