Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amandus Julius Chinguile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nachingwea
Primary Question
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mfumo utakaowezesha kupata idadi sawa ya nafasi za ajira katika kila Jimbo badala ya mfumo wa sasa?
Supplementary Question 1
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Spika, nipongeze kwanza Serikali, wamesema sasa walau wameshusha kwa ngazi ya mkoa, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza: Je, Serikali haioni iko haja sasa ya kutambua mahitaji ya nafasi hizi za kazi kwa kila jimbo ili kutoa msawazo sawa na baadaye kuratibiwa kitaifa ili kulinda utaifa? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, wako vijana ambao walihitimu vyuo mbalimbali kuanzia 2015 mpaka 2020 na kwa sasa kwa kutumia mfumo hawa vijana ni kana kwamba mfumo unawakataa. Je, Serikali haioni iko haja sasa ya kutoa upendeleo maalum kwa hawa vijana ambao kwa sasa kwa sababu ya umri unavyokwenda wanaachwa sasa kwenye mfumo wa ajira? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Amandus kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza ametaka kujua kwamba Serikali ina mpango gani wa juu ya kushusha hizi ajira katika ngazi ya majimbo kwa maana hiyo. Bunge lako Tukufu lilitoa maelekezo kwa Serikali kwamba wahakikishe ajira hizi zinashuka katika ngazi za mikoa. Katika kutekeleza hilo na commitment ambayo Serikali ilitoa ndani ya Bunge hili, tayari utekelezaji huo umeanza ambao tumeanza katika ngazi ya mkoa na usaili utafanyika katika ngazi ya mkoa ambapo utahusisha Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zetu.
Mheshimiwa Spika, baadaye kwa kuwa safari ni hatua, tayari Serikali itaendelea kujipanga kwa namna ya kushuka katika ngazi ya wilaya. Kwa hiyo, nimwondolee shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imekuwa ikisikiliza maelekezo ya Bunge na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge na ushauri wake tunaupokea, tutaingiza katika utekelezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ameuliza habari ya kwamba ni namna gani Serikali imejipanga sasa kuangalia wale waliohitimu kwa miaka ya nyuma. Ni kweli katika nyakati mbalimbali Serikali imetumia hiyo approach ya kuchukua wale wa miaka ya nyuma na ndani ya Bunge humu tulipata ushauri huo, lakini kiukweli ukiangalia wale wanaohitimu na namna ambavyo Serikali imekuwa ikitoa ajira nafasi zinakuwa ni chache. Kwa hiyo, ukienda kwa mtindo huo unaweza ukakuta tunakaa ndani ya mwaka mmoja.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka mmoja, kwa mfano waliohitimu 2015 tunakaa tunaajiri ndani ya miaka sita, kwa hiyo, tatizo litakuwa pale pale, ndiyo maana tumerejea kufuata kwenye Sera ya Ajira na Utumishi kwamba sasa waende kwenye ushindani na katika ushindani ili kuzingatia pia waliomaliza kwa miaka ya nyuma, Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kwamba kama endapo waliokuwa kwenye ushindani wamefungana kwa marks na yule ambaye ana umri mkubwa atapewa kipaumbele, nashukuru. (Makofi)
Name
Eng. Ezra John Chiwelesa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Primary Question
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mfumo utakaowezesha kupata idadi sawa ya nafasi za ajira katika kila Jimbo badala ya mfumo wa sasa?
Supplementary Question 2
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kumekuwa na taratibu zile kwa mfano nafasi za majeshi na vitu vingine ambavyo watoto wanapatikana kwenye maeneo yetu ya majimbo. Baada ya usaili kutoka kwenye wilaya, anafika mkoani mkoa wanawarudisha, wanaambiwa huyu ana kovu, sijui ana nini, kumekuwa na vigezo vingi sana watu wa mkoa wanadhulumu watu wa wilaya.
Mheshimiwa Spika, sasa tulikuwa tunaomba nafasi zipelekwe wilayani hasa zile ambazo hazihitaji vigezo zaidi ya Form Four. Wakishatoka wilayani waende moja kwa moja kwenye training kwa sababu wanapofika mkoani, watu wa mkoani wanakuwa na nafasi za kuchomeka watu wao na watu wetu waliotoka kwenye wilaya wanaachwa. Tulikuwa tunaomba hilo lizingatiwe, ni hilo tu. (Makofi)
Name
Dr. Tulia Ackson
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mbeya Mjini
Answer
SPIKA: Ahsante sana, nadhani huo ulikuwa ni ushauri, kwa hiyo, utachukuliwa halafu wakaupime kwa sababu hapo mwishoni umemaliza vizuri, lakini vigezo lazima vizingatiwe. Tukisema kutakuwa hakuna vigezo kwa sababu tu watu wametoka mahali, itakuwa changamoto, ila mwishoni umemaliza kwamba unatoa ushauri wa namna ambavyo wafanye hili zoezi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Naibu Waziri naamini umeupokea huo ushauri.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mfumo utakaowezesha kupata idadi sawa ya nafasi za ajira katika kila Jimbo badala ya mfumo wa sasa?
Supplementary Question 3
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nilitaka nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba je, wapo tayari kutoa hadharani vigezo wanavyotumia kwa vijana kupata ajira ili kuondoa usumbufu wa vijana wanaoomba ajira, kusumbua Wabunge wakidhani kwamba ukituma message kwa Mbunge atakuombea ajira ili wajue kwamba ajira inatolewa kwa haki na mtu atakayeomba ana sifa atapata nafasi hiyo, ahsante.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Ni wazi kwamba kupitia Sekretarieti ya Ajira, vigezo vyote viko wazi na kwa namna ambavyo tunafanya usaili, matokeo yanatoka wazi na wale ambao wanatokea kukosa wanapewa sababu. Hata hivyo, tumetoa fursa ya kwamba yule ambaye anadhani hakutendewa haki, amepewa fursa ya kukata rufaa. Kwa hiyo, vigezo vyote viko wazi na kila Mtanzania yuko wazi kuomba kwa kadri ya nafasi anayotaka, nashukuru. (Makofi)
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mfumo utakaowezesha kupata idadi sawa ya nafasi za ajira katika kila Jimbo badala ya mfumo wa sasa?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tulikuwa tunajadili suala la wale vijana ambao wanajitolea kwenye shule zetu kufundisha au kutoa huduma kwenye vituo vya afya. Serikali imekuwa inaahidi kwamba itatoa kipaumbele wakati wa kutoa ajira kwa hawa wanaojitolea. Je, Serikali imechukua hatua gani angalau kuchukua kuunda kanzidata ya hawa vijana wanaojitolea? Mimi najua kwamba watu wa Jimbo la Vunjo iliwasilisha orodha ndefu tu ya vijana wanaojitolea, naomba kupewa jibu.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali hilo la Mheshimiwa Dkt. Kimei kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka utaratibu mzuri katika ajira safari hii. Kweli vijana wanaojitolea katika sehemu zetu huko katika Serikali ni wengi, tumechukua kanzidata na tukaona kwamba suala la wanaojitolea halitakuwa automatic, nao wataingia kwenye mfumo wa ushindani, lakini mwishoni yule aliyejitolea atakuwa na added advantage ukilinganisha na yule asiyejitolea.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali inaandaa mfumo mzuri ambao tutawabaini kwanza namna ya kuwapata hao wanaojitolea na pia hawa wanajitolea wamekuwa wakifanya kazi pia kuona namna hata ya kuwapatia stahiki ili waweze kupata morali ya kuweza kujitolea. Kwa hiyo, Serikali ina utaratibu mzuri na tumeshauandaa hivi karibuni tutau-submit. (Makofi)
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza: - Je, Serikali haioni haja ya kuanzisha Mfumo utakaowezesha kupata idadi sawa ya nafasi za ajira katika kila Jimbo badala ya mfumo wa sasa?
Supplementary Question 5
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, kwa sababu tatizo la ajira mpya kuhama kwenye Halmashauri zile za pembezoni limekuwa ni kubwa sana, nini kauli ya Serikali juu ya watumishi hawa ambao wanaajiriwa baada ya miaka mitatu wote wanakuwa wameondoka kabisa kwenye vituo vyao vya kazi? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeweka utaratibu mzuri kwamba mtumishi anapoajiriwa anatakiwa kukaa kwenye kituo cha kazi miaka isiyopungua mitatu. Hata hivyo, kuna taratibu mbalimbali ambazo ni miongozo kwamba hata kuomba uhamisho na sasa hivi tumeanzisha mfumo mzuri ambao waajiri wanaomba uhamisho kupitia kwenye mfumo unaitwa e-Uhamisho.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge na hata katika ajira hizi tulizotangaza zimetangazwa kimkoa. Naomba niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba baadhi ya kada za afya hasa mikoa ile ya pembezoni zimekosa wanaoomba, nafasi ni nyingi lakini wanaoomba wamekuwa wachache hasa mikoa ya pembezoni mfano Mtwara, Kigoma na Mkoa wa Lindi.
Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa waombaji wasikimbilie tu kuomba nafasi hizi sehemu za mijini kwa sababu huko kuna ushindani mkubwa. Niwaase pia waombe huko kwa sababu pia Serikali imeweka vizuri miundombinu kama vile maji na huduma nyingine za kijamii. Kwa hiyo, wasihofu kuomba ajira katika sehemu za mikoa ya pembezoni, nakushukuru.