Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:- Je, faida gani Serikali imepata kwa kuanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja bila kusubiri mingine ikamilike ili kuanza mipya?
Supplementary Question 1
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Swali langu, kipi kimekuwa kipaumbele cha Serikali katika kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa sababu miradi mingi imekuwa inaanzishwa lakini haikamiliki, lakini pengine mingine inatelekezwa na ku-attract interest. Mfano mdogo ni mradi wa masoko ya kimkakati ulioko Kyerwa, Mulongo pia Nankwenda umetelekezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila kuguswa na kufanya chochote ikiwa imefikia linta.
Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza. Katika miradi ambayo inachukua muda mrefu na ku-attract interest, lakini mingine imetelekezwa na ikiwa imekopewa fedha, ni ipi thamani ya fedha katika miradi ya namna hiyo? (Makofi)
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, miradi hii ya kipaumbele nimweleze tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mipango yote ambayo inakwenda kutekelezwa na Serikali inazingatia mambo mengi. Moja, kama nilivyoeleza katika majibu ya msingi ni kuangalia ile miradi wezeshi ambayo inakwenda kuchochea maendeleo katika sekta nyingine.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, miradi yote inayoanzishwa inakuwa imefanyiwa study na ina umuhimu wake na ndiyo maana imeanzishwa kwa kila eneo. Kwa hiyo, kwa mfano hili la Kyerwa nadhani labda tulifanyie ufuatiliaji wa karibu, tujue tatizo nini? Pia kuwepo na soko katika eneo la Kyerwa ni mahali pazuri kwa wafanyabiashara na wakulima kupelekeza mazao yao kwa ajili ya kwenda kuuza na wale wanaonunua kama ni jumla, basi waende wakauze rejareja katika maeneo mengine. Hii yote ni katika mnyororo wa thamani katika kuongeza thamani na kuweza kuongeza uchumi kwa wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, vilevile katika swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anasema miradi imetelekezwa. Inawezekana kweli unasema imetelekezwa kwa sababu ya mtazamo unaoona, lakini hakuna mradi hata mmoja uliotelekezwa, miradi yote inategemea upatikanaji wa fedha. Sasa inapotokea kwamba kuna changamoto ya upatikanaji wa fedha, miradi hiyo inaonekana kama imesuasua au imetelekezwa lakini upatikanaji wa fedha unapopatikana basi miradi hiyo inaendelea kutekelezwa na inakwenda ku-service au yale makusudi yaliyokusudiwa inapokuwa imekamilika, basi maendeleo yanakuwa yanaendelea kutokana na mahitaji ambayo yamepangwa katika mradi huo.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Name
Halima James Mdee
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:- Je, faida gani Serikali imepata kwa kuanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja bila kusubiri mingine ikamilike ili kuanza mipya?
Supplementary Question 2
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, moja kati ya miradi mingi ambayo inaanzishwa kwa pamoja ni miradi ya barabara. Ninavyozungumza sasa hivi barabara mbalimbali wakandarasi wameondoka site kwa sababu ya madeni. Hadi mwezi Machi, wakandarasi washauri waelekezi walikuwa wanaidai Serikali shilingi bilioni 913 ikiwa ni pamoja na riba ya shilingi bilioni 79.5. Kamati ya Bunge ya Bajeti ilishaishauri Serikali...
SPIKA: Mheshimiwa Halima ni kwenye swali siyo uchangiaji, uliza swali.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, Serikali inadaiwa na wakandarasi kiwango cha fedha nilichokitaja pamoja na interest imesababisha barabara nyingi zimekwama. Ni lini mtajenga barabara kutokana na uwezo wa Serikali wa kibajeti? (Makofi)
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mdee kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tunapitisha bajeti katika Bunge lako Tukufu na tunapopitisha bajeti, lengo la Serikali ni kwenda kutekeleza miradi yote ambayo imepitishwa katika bajeti. Hata hivyo, tatizo linapotokea kwamba kuna wakati labda fedha zinachelewa kutoka au kwa sababu moja au nyingine aidha ni ya kimfumo au sababu nyingine yoyote inasababisha miradi hiyo kusuasua na kuchelewa.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali tumejipanga na Serikali iko tayari kupitia Wizara ya Fedha tunakwenda kutoa fedha kwa ajili ya kulipa madeni na kwenda kuzuia yale maongezeko ya riba katika miradi mbalimbali. Kwa hiyo, tutakwenda kutoa fedha kwa wakati ili kuweza kuzuia ongezeko la riba katika mikataba mbalimbali ya wakandarasi. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali iko makini na tunakwenda kuhakikisha miradi hiyo inakwenda kukamilika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved