Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama za kusafisha figo kupitia Bima ya Afya kwa Wote?

Supplementary Question 1

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, kwanza, naishukuru Serikali kwa hatua inayochukua. Kwa kuwa sasa Watanzania wengi wanakabiliwa na kadhia hii, je, Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka wa kutazama upya gharama hii ambayo kwa wiki pengine ni kati ya shilingi 600,000 mpaka shilingi 800,000 na ukifikiria kwa mwaka mzima wenye majuma 52 gharama hii hailingani kabisa na mapato ya Watanzania?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali ina mkakati gani sasa wa kwenda kwenye ngazi ya vituo vya afya tulivyojenga ili kupunguza gharama hii na kuweza kununua vifaa pamoja na kuwaandaa wataalamu ili kupunguza gharama hii kwa Watanzania wanaopitia wakati huu mgumu wa matibabu kwa gharama hizi kubwa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kutizama eneo hili muhimu ambalo linawagusa Watanzania wengi.

Mheshimiwa Spika, moja, Serikali imeshaanza na ndiyo maana kama mlisikia juzi moja ya hospitali sasa hivi wameshusha zile gharama ulisikia kwamba unakuta shilingi 250,000 mpaka shilingi 300,000 kwenye maeneo mengine, sasa hivi ukienda kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam ni shilingi 150,000. Kwa hiyo, gharama inaendelea kushuka kutokana na hatua hizi ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, kwamba twende kwenye ngazi ya zahanati na mambo mengine, kwanza suala hilo linahitaji investment kubwa na utaalamu. Sasa hivi tuko kwenye ngazi ya mkoa. Tutaendelea kujipanga kwa namna ya kushuka kwenye ngazi ya wilaya jinsi muda unavyokwenda, lakini kwanza tujenge uwezo kwenye ngazi ya mkoa.

Mheshimiwa Spika, pia namuomba Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wenzangu, suala siyo tunatibuje figo mara matatizo yatakapotokea, lakini tujikite kuzingatia yale ambayo Profesa Janabi na wataalamu wengine wanasema ili tusiweze kupata matatizo ya figo. (Makofi)

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama za kusafisha figo kupitia Bima ya Afya kwa Wote?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Kwa kuwa magonjwa haya yasiyoambukiza ikiwemo figo, Naibu Waziri amezungumza kwamba Hospitali ya Temeke inafanya matibabu kwa shilingi 150,000/=: Kwa nini isipungue kwa Taifa zima ili na watu wa mikoa mingine waweze kuhudumiwa? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mwakagenda. Ni kweli lengo ni kwenda nchi nzima, lakini kwa sababu tunaendelea kwa maana ya kubadilisha vifaa kwenda kwenye vitendanishi, tuna-rollout nchi nzima. Bado naendelea kusisitiza, suala la magonjwa ambukizi tuzingatie maelekezo ya Profesa Janabi na wataalam wengine, hapo ndipo tutakapoweza kutoka.