Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Primary Question

MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kudhibiti wimbi la Wahamiaji haramu katika Mipaka ya nchi yetu?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wahamiaji haramu bado wamekuwa wakionekana wanaingia nchini na wanapopatikana wanapelekwa katika Magereza yetu ambako wanaongeza gharama za bajeti katika Magereza yetu: Je, Serikali haioni haja ya kuwarejesha kwao mara tu wanapowakamata? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Othman, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli wapo wahamiaji haramu ambao wanapokamatwa hurejeshwa kwenye nchi zao, lakini wapo ambao wakati tunafanya mawasiliano na nchi zao, huwekwa Magerezani na wapo wanaofungwa kutokana na aina ya makosa waliyoyatenda, ahsante sana.