Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kufanya maboresho ya minara iliyojengwa na Halotel Liwale ili iweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa?

Supplementary Question 1

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri yanayoonesha uwajibikaji wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; vipo Vijiji vya Gongowele, Mirui, Kimambi na Mpigamiti, minara ile inatumia umeme jua (solar). Je, Serikali iko tayari kutubadilishia nishati ili minara hii iweze kufanya kazi masaa 24? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; hivyo Vijiji vya Ndapata, Kikulyungu na Ndunjungu, vijiji hivi havina mawasiliano kabisa. Je, ni nini kauli ya Serikali kuwapatia mawasiliano wananchi hawa? (Makofi)

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zuberi Mohamedi Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli na bahati nzuri nimefika katika maeneo ya jimbo lake ikiwemo Mpigamiti ambayo ameitaja, ambako kuna minara ilijengwa na bahati mbaya wakati huo huduma ya umeme ilikuwa haijafika kwenye hayo maeneo, kwa hiyo, tukaweka solar.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa solar ina changamoto, wakati mwingine kama hakuna jua la kutosha kunakuwa hakuna nguvu ya umeme wa kusukuma hiyo minara. Nimeelekeza na hapa nataka kusisitiza maelekezo haya, maeneo yote ambapo umeme wa REA umefika, minara ya maeneo hayo inapaswa kuunganishwa na umeme ili wananchi wapate huduma wakati wote na kule ambako huduma ya umeme haijafika tuweke jenereta kwenye hiyo minara ili huduma ya wananchi isikatike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, vijiji alivyovitaja, kweli ni katika vijiji ambavyo huduma hii haijafika, lakini namhakikishia Mheshimiwa Kuchauka kwamba, tathmini imefanyika na katika awamu inayofuata ya ujenzi wa minara tutaviingiza vijiji alivyovitaja ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma wanayostahili kupata. (Makofi)