Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, ni sababu zipi zinasababisha wakulima wa tumbaku kukopeshwa pembejeo na kuuza tumbaku kwa Dola badala ya shilingi ya Tanzania?
Supplementary Question 1
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, kwa vile biashara yote ya tumbaku inalipwa kwa dola, kwa nini wakulima wanalipwa kwa shilingi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tumbaku inafanyika kwa dola na kinachofanyika ni kwamba transaction inapotoka kwa mnunuzi kwenda kwenye vyama vikuu vya msingi huwa vinafanyika kwa dola. Inapotoka kwenye transaction kutoka katika vyama vya msingi baada ya makato yote ambayo wakulima wanakuwa walikopa katika msimu wa kilimo, ile difference inayobaki wakulima wanalipwa kwa shilingi kulingana na thamani ya fedha ya siku hiyo husika. Hicho ndicho ambacho kinafanyika sasa. Ahsante sana.
SPIKA: Sasa huyo anayebadilishia hapo katikati ni nani kama mkulima huwa anapata pembejeo kwa dola na yule mnunuzi ananunua kwa dola, nani anayembadilishia mkulima hapo ghafla kwamba yeye ndiyo apewe shilingi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni Chama Kikuu cha Msingi (TCJE) ambao sasa wao ndiyo wameingia mikataba na wakulima kwa sababu zile account za wakulima ni za shilingi. Kwa hiyo wao wanachokifanya wana-convert ile thamani ya dola ya siku hiyo; yaani kwa mfano labda mkulima thamani yake labda ni dola 100 kwa hiyo wanakwenda kuangalia katika thamani ya bei ya shilingi ya dola kwa siku hiyo kama ni 2,500, kwa hiyo watalipwa ile shilingi 250,000/=, lakini hiyo inatoka kwenye Chama cha Msingi, Chama Kikuu cha Ushirika kwenda kwa mkulima.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, ni sababu zipi zinasababisha wakulima wa tumbaku kukopeshwa pembejeo na kuuza tumbaku kwa Dola badala ya shilingi ya Tanzania?
Supplementary Question 2
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nataka kujua kwa kuwa Mkoa wa Mara, Wilaya ya Serengeti imekuwa ikilima zao la tumbaku sana na sisi Jimbo la Bunda kuna maeneo yanayofanana na Serengeti. Je, ni lini sasa Serikali itapeleka wataalam wa kupima ule udongo wa Jimbo la Bunda ili waweze kulima zao la tumbaku? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge Mwita Getere kwamba mara baada ya Bunge letu la mchana nitakwenda kuzungumza na wataalam ili tuweze kutuma wataalam katika eneo lake waweze kupima na kuona kama linafaa. Kwa hiyo tutalifanya hilo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved